• Latest News

  April 04, 2016

  Magufuli afuta sherehe za sikukuu ya muungano  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.

  Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

  Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Chato
  04 April, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Magufuli afuta sherehe za sikukuu ya muungano Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top