• Latest News

  April 09, 2016

  Rais Magufuli Amteua Bwana G. Byakanwa Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Hai


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

  Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016. Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

  Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  08 Aprili, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli Amteua Bwana G. Byakanwa Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Hai Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top