• Latest News

  April 14, 2016

  Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mhariri Mtendaji Wa Magazeti Ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.

  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

  Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu
  nafasi hiyo.

  Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam-14 Aprili, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mhariri Mtendaji Wa Magazeti Ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top