Header Ads

Magufuli amemteua Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi wa CDA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).

Taarifa iliyotolewa jana  tarehe 20 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Paskasi Muragili umeanzia tarehe 17 Februari, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Mhandisi Paskasi Muragili alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), nafasi aliyoichukua kuanzia mwaka 2012.

No comments