• Latest News

  April 21, 2016

  RASMI YANGA YAPANGWA NA TIMU KUTOKA ANGOLA KATIKA CAF


  Baada ya Yanga kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri na hivyo kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, timu hiyo ya Jangwani sasa imepangiwa timu kutoka Angola katika Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano.

  Kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) zinaeleza kuwa timu ambazo zitatolewa katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitashuka katika Kombe la Shirikisho ambapo huko zitakutana na timu nane zilizosonga mbele ambapo zitacheza mechi za mtoano za nyumbani na ugenini kisha zitakazofuzu zitaingia hatua ya makundi.

  Baada ya Yanga kutolewa, sasa itakutana na Sagrada Esperança baada ya droo kupangwa jana huku Yanga ikitakiwa kuanzia nyumbani wiki ya Mei 6-8, mwaka huu na marudio ni Mei 17-18, 2016.

  RATIBA KAMILI YA MTOANO KOMBE LA SHIRIKISHO IPO HIVI: 


  MO Béjaïa (Algeria)     Vs     (Tunisia) Espérance de Tunis Stade Malien (Mali)    Vs        (Morocco) FUS Rabat
  Étoile du Sahel (Tunisia)     Vs    (Gabon) CF Mounana
  TP Mazembe (DR Congo)     Vs    (Tunisia) Stade Gabèsien
  Al-Ahli Tripoli (Libya) Vs         (Misri) Misr El-Makasa
  Al-Merrikh (Sudan)     Vs    (Morocco) Kawkab Marrakech
  Young Africans (Tanzania)     Vs    (Angola) Sagrada Esperança
  Mamelodi Sundowns (Sauz) Vs     (Ghana) Medeama
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RASMI YANGA YAPANGWA NA TIMU KUTOKA ANGOLA KATIKA CAF Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top