Header Ads

ROBOTI WA KIKE ATENGENEZWA CHINA

 Pichani: Roboti wa kike, Jia Jia ni huyo mwenye nguo nyekundu.
Unaweza kushangaa lakini ndiyo ukweli wenyewe kwamba jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Chen Xiaoping amefanikiwa kutengeneza roboti wa kike na kumpa jina la Jia Jia lenye maana ya mungu roboti wa kike.
Chen Xiaoping anasema kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akiwaona watu wakitengeneza maroboti wenye vyuma hivyo alichokuwa akifikiria ni kutengeneza roboti na kisha kumvisha ngozi, aonekane kama binadamu, na kweli akafanikiwa kwa asilimia kubwa.
Ukimwangalia roboti huyu, ni vigumu kumgundua kwani ana kila kitu kwa nje ambacho binadamu wa kawaida anacho. Lengo lake la kutengeneza roboti huyo hakusema, kama ni kufanya kazi au vitu vingine ila kitendo cha kutengeneza roboti huyo kimempa heshima kubwa kijana huyo aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia hapohapo China.
Umejifunza nini? Je kuna siku na sisi Waafrika tutafika huko?
Unaweza kushare na wenzako...
Source: Daily Mail, England.

No comments