Header Ads

Ruby, Maua Sama uso kwa uso na Ne-Yo, Mwanza

 Staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’.
Mau Sama Global TV Online (3)Maua Saleh ‘Maua Sama’.
Na Andrew Carlos
WAKALI wa sauti za kumtoa nyoka pangoni, Maua Saleh ‘Maua Sama’ pamoja na Hellen George ‘Ruby’ wanatarajiwa kukutana uso kwa uso na staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’, katika bonge la shoo litakalofanyika Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
ruby 
Hellen George ‘Ruby’.
Akizungumza na Over Ze Weekend, mratibu wa shoo hiyo inayotambulika kama Jembeka Festival 2016, Sebastian Ndege alisema kuwa mbali na Maua na Ruby, usiku huo utakuwa pia maalum kwa mastaa kibao wakiongozwa na Diamond Platnumz.


“Historia inatarajiwa kuweka jijini Mwanza kwa Ne-Yo kupiga shoo ya laivu kwa kutumia vyombo huku mastaa kibao kutoka Bongo wakimsindikiza ambao ni Mo Music, Mr Blue, Fid Q, Stamina, Nay wa Mitego na wengineo,” alisema Sebastian. Shoo hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom pamoja na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.

No comments