Header Ads

Serikali yakiri upungufu wa sukari, yaagiza nje ya nchiKwa ufupi
Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.
Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.
 

Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.
 

Alisema takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani 37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.
 

“Ninawaagiza maafisa wa biashara kushughulikia suala hili, na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu  tulizojiwekea,”  alisema Majaliwa.
Mwananchi iliibua suala hilo baada ya kutoa ripoti maalum wiki iliyopita inayoonyesha kuwa kilo moja ya sukari inauzwa kati ya Sh2,200 na 2,500 tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.


CHANZO:By Peter Edson, Mwananchi Digital

No comments