Header Ads

Shamsa, Faiza washerehekea kulea wenyewe!

 
 Shamsa Ford
 KITUKO: Kweli? Mastaa wawili wa Bongo Muvi, Shamsa Ford na Faiza Ally wametamba kuwa wanasherekea maisha ya ‘usingo mama’ wakidai wanalea wenyewe watoto wao bila wazazi wenzao.
Wakizungumza na Wikienda kwa pamoja wakiwa kwenye viwanja vya bata jijini Dar, Shamsa na Faiza walidai kuwa, pamoja na wazazi wenzao kukaa pembeni na kuwaachia majukumu ya kulea, ‘wanainjoi’ na kwamba wao ni mfano wa wanawake wanaojiamini.
IMG_1413
“Sisi ni ‘singo mama’, tunasherehekea kulea wenyewe, hili ni jeshi kamili halimtegemei mtu,” alisema Shamsa anamlea mwanaye Terry aliyezaa na Dickson Matok ‘Dick’ huku Faiza anayeishi na mwanaye Shasa aliyezaa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akidakia huku wakigonganisha viganja: “Tunasherekea kuwa singo mamaa...”
Kwa upande wao, Dick na Sugu hawakupatikana ili kusikia upande wao juu ya ishu hiyo hivyo jitihada zinaendelea.
 IMG_1415

 Stori:  Imelda Mtema, Wikienda/GPL

No comments