• Latest News

  April 02, 2016

  Shamsa: Nusura niharibike ubongo kwa kipigo  Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.

  Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo.
  Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki.
  “Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Shamsa: Nusura niharibike ubongo kwa kipigo Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top