• Latest News

  April 04, 2016

  TAARIFA YA MSIBA WA PADRE FABIAN NDERUMAKI WA JIMBO LA KATOLIKI MOSHI


  Mhashamu Askofu Izaac Amani wa jimbo katoliki la Moshi kwa masikitiko na huzuni kubwa, anatangaza kifo cha mheshimiwa sana padre FABIAN NDERUMAKI (pichani), Padre wa jimbo la Katoliki la Moshi.

  Padre Fabian Nderumaki, ambaye alifariki dunia jana saa nne usiku hadi mauti yanamfika alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Himo jimboni Moshi.

  Kabla ya kuteuliwa na baba askofu kuwa paroko wa Himo, Padre Fabian Nderumaki alikuwa Gombera (Rector) wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yakobo-Kilema (St. James Seminary)

  Tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa, marafiki, wote waliofanya naye kazi seminari ya St. James na waumini wote ambao Padre Fabian Nderumaki amewahi kuwahudumia katika parokia zao kama padre enzi za uhai wake. Pia kwa mapadre, watawa na wote waliowahi kufanya nae kazi

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa,

  Jina la Bwana libarikiwe milele na milele, AMINA.

  ROHO YA MAREHEMU PADRE FABIAN NDERUMAKI IPATE REHEMA KWA MUNGU, APUMZIKE KWA AMANI.

  R.I.P OUR BELOVED REV. FATHER FABIAN NDERUMAKI.

  UPDATES ZA MSIBA

  Marehemu Padre Fabian Nderumaki anatarajiwa kuzikwa Ijuma tarehe  April 8, 2016  Ijumaa.

  Misa itaanza saa 5:00 katika Kanisa la Mt. YOSEFU Longuo, Moshi.

  Mipango ya mazishi kwa hapa Dar es salaam  inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Gabriel Nderumaki Kimara Temboni.

  Kwa mawasiliano zaidi piga:

  namba 0713 323762 (Gabriel Nderumaki) na 0715 433739(Adam Nderumaki)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TAARIFA YA MSIBA WA PADRE FABIAN NDERUMAKI WA JIMBO LA KATOLIKI MOSHI Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top