• Latest News

  April 26, 2016

  Tanzia: Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki Afariki Dunia


  Mke wa Rais mstaafu  wa    Kenya, mama Lucy Kibaki amefariki dunia . Lucy alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London alikokuwa amelazwa.

  Alisafrishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.

  Akithibitisha kifo chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.

  Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .

  Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.

  Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.
  Chanzo:BBC 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tanzia: Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki Afariki Dunia Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top