Header Ads

Wanamuziki, wadau kukutana na Makonda kesho

WANAMUZIKI wa dansi, taarab, Bongo Fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda, ili kubadilishana mawazo juu mwenendo wa kazi zao.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa tano ili kujadili changamoto za Sheria ya Biashara ya Vileo na Burudani ambayo iko tangu mwaka 1968 na 1972.

Mmoja wa wasemaji wa umoja huo, Juma Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa maombi yao ya kumwalika Makonda yameshawasilishwa kwake.

Mbizo amesema mkutano huo hauhusiani na chama chochote cha muziki, bali umeandaliwa na waathirika wakuu wa sheria hiyo.

No comments