Header Ads

Wanatisha kwa mkwanja lakini historia ya maisha yao unaweza kulia

NEW YORK, Marekani
BAADA ya dhiki faraja. Msemo huu wa wahenga umezoeleka kutumika katika jamii ya Tanzania ukiwa na maana kwamba, baada ya mtu kupitia katika kipindi kigumu hatimaye hupata mafanikio.
Msemo huu haitakuwa vibaya kama utautumia kwa mastaa hawa ambao ukiangalia historia waliyopitia katika maisha yao ilikuwa ni ya kutisha, iliyojaa umasikini wa kutupwa, lakini pamoja na hali hiyo, kwa sasa wanakula ‘bata’.
Mastaa hao 10 walioibuka baada ya kuishi katika familia zilizojaa msoto kimaisha ni kama ifuatavyo:
 10. Sarah Jessica Parker
INAWEZA kuwa vigumu kuamini kwamba, Sarah Jessica Parker, ambaye ni mwanamke aliyetunga na kuandaa kipindi cha Carrie Bradshaw, kilichotamba katika  vituo vya televisheni katika onesho la Sex and the City kwa muda wa miaka sita, alitokea katika umasikini wa kutupwa.
Parker alikulia katika kitongoji cha Nelsonville, Ohio na mwaka 2000 aliwahi kuliambia  gazeti la New York Times  kuhusu maisha ya utotoni kwake.
“Tulikuwa tunaishi katika nyumba za umma. Nakumbuka tulikuwa tunaishi katika umaskini wa kutupwa. Hakuna njia sahihi ya kulificha hilo. Wakati mwingine hatukuwa na umeme. Wakati mwingine hatukuweza kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi, wakati mwingine pia hatukuweza kuadhimisha siku ya kuzaliwa ama kulipa bili za umeme,” alieleza katika mahojiano na gazeti hilo.
“Hatukuwa na uwezo wa kulipia pia bili za simu, ilikuwa inatulazimu kuzima simu, tulikuwa tunabaki kimya na kumuangalia mama ama wazazi hatua watakazochukua, wazazi wangu walikuwa wakihangaika  kutafuta fedha,” alisema  Sarah, ambaye ni mmoja kati ya watoto nane ambaye alikuwa akilelewa na baba wa kambo akiwa na mzigo wa familia.
Baada ya msoto huo wa kimaisha kwa sasa mwigizaji huyo anasemekana kuwa na utajiri ambao unazidi dola milioni 90.
Leonardo Dicaprio 
9. Leonardo Dicaprio
Katika siku hizi, Leonardo Dicaprio anaishi katika jumba la kifahari na anamiliki ndege binafsi, lakini Dicaprio hadi sasa mara zote huwa hayasahau maisha yake ya mwanzo. Kabla ya kutumbukia katika Kijiji cha Hollywood, Leo alikuwa mtoto masikini akiishi katika eneo la Los Angeles, ambalo lilikuwa limezungukwa  na wauza dawa za kulevya na makahaba.
Februari  2014 Dicaprio aliliambia gazeti la Los Angeles Times alikulia katika umasikini katika eneo lililopo karibu na jiji  la  Los Angeles.
Alisema kwamba, jamii ya wauza unga na makahaba ndio walikuwa wamemzunguka, jambo ambalo lilimfanya kufahamu madhara ya dawa za kulevya akiwa katika umri mdogo kutokana na kwamba alikuwa akiwashuhudia waathirika wakiwa wamemzunguka.
Akiwa na umri wa miaka 41, mwigizaji huyo anadai kuwa na utajiri unaokadiriwa kuzidi dola milioni 200 na sasa anaishi maisha ya kifahari.
  1. Tom-CruiseTom Cruise
Tom Cruise alizaliwa mwaka 1962  katika eneo la Syracuse, New York. Baba yake mzazi alikuwa mhandisi wa umeme na mama yake alikuwa mwalimu wa elimu maalumu. Pamoja na baba yake kuwa na uwezo, alikuwa haijali na matokeo yake ikawa masikini. Akiwa na umri mdogo, Cruise  alivutiwa na fani ya uigizaji na alikuwa akishiriki tasnia hiyo akiwa shuleni. Akiwa na umri wa miaka 11 mama yake alitengana na baba yake na baadaye mwaka huo baba yake alifariki kwa ugonjwa wa saratani.
Kutokana na hali hiyo, katika kipindi cha ujana wake ilimlazimu mama yake Tom kufanya kazi nne tofauti ili kuweza kuwasaidia watoto wake wanne. Hali hiyo pia ilimlazimu Tom kuachana na masomo ya sekondari kwa ajili ya kuendelea na kazi ya uigizaji.
Kutokana na umahiri wake, mwaka 1983, Tom alionekana katika filamu za The Outsiders, Risky Business na All the Right Moves.
Hata hivyo, nafasi  aliyocheza kwenye filamu  ya Top Gun mwaka 1986 ndiyo iliyomfanya aanze kuwa staa katika Kijiji cha Hollywood.
Utajiri  wa Tom Cruise kwa sasa unakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola milioni 500.
7. Hilary Swank
Mshindi huyo mara mbili wa tuzo  za Oscar, Hilary Swank alikuwa katika eneo la kimasikini katika jiji la Washington.
Baba yake Swank alitelekeza familia yake wakati nyota huyo akiwa mdogo na hivyo kumfanya alelewe na mama yake wakiwa watoto wawili. Akiwa na umri wa miaka 15, Hilary aliachana na shule na mwaka huo huo mama yake akapoteza kibarua na hivyo kuifanya familia kufungasha mizigo  na kuhamia California, huku Hilary akiwa na ndoto zake za kuwa mwigizaji.
Katika kipidi hicho walikuwa wakilala ndani ya gari lao na mchana wakishinda kwenye nyumba za marafiki zao hadi walipoweza kupata uwezo wa kukodi nyumba. Hilary aliweza kushiriki katika maeneo mbalimbali ya filamu, lakini hakuweza kutamba hadi mwaka 1999 alipokuja kutamba katika filamu ya Boys Don’t Cry .
Vilevile alikuwa akiingiza kitita cha dola 75 kwa siku wakati wakitayarisha filamu hiyo ya  Boys Don’t Cry, ambapo aliweza kuingiza jumla  ya dola 3,000.
Kwa sasa  Swank anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola zaidi ya milioni 40.
  1. Jim Carrey
Jim Carrey 
Jim Carrey alizaliwa katika mji wa  Ontario, Canada na ni mtoto  wa mwisho kati ya wanne. Carrey alikulia katika familia ya maisha ya watu wa kati hadi baba yake alipopoteza  kazi wakati huo staa huyo akiwa kijana.
Kutokana na hali hiyo, iliifanya familia kuanza kuishi katika maisha magumu na hatimaye wakapoteza nyumba na hivyo wakalazimika kuanza kuishi ndani ya lori.
Hali hiyo ndiyo iliyomlazimu Jim kuachana na shule akiwa na umri wa miaka 15 ili aweze kufanya kazi muda wote kwa ajili ya kusaidia familia yake. Alikuwa akifanya kazi ya ulinzi na ya kufungua mageti. Baadaye familia yake ilisimama tena na Carrey akaanza kuigiza vichekesho wakati akijaribu kujitafutia jina.
Akiwa katika harakati hizo alikuja kugunduliwa na mchekeshaji Rodney Dangerfield ambaye alimsaidia Jim  hadi akaweza kusimama mwenyewe.
Licha ya kupata  umaarufu katika tasnia hiyo ya uigizaji, Carrey  hakuachana na dhamira yake ya kutengeneza filamu na vipindi vya televisheni ambapo baada ya  mwaka 1990  kupewa nafasi kuigiza katika kipindi cha  In Living Color, hapo ndipo kazi ya Jim ilipoanzia. Kwa sasa staa huyo anakadiriwa kuwa na utajiri unaozidi dola milioni 150.
Hata hivyo, pamoja na utajiri huo, kazi ya kufungua mageti, ulinzi na kulala kwenye lori ni  mambo ambayo hayajaondoka kichwani mwa mwigizaji huyo.
  1. Demi Moore
Demi Moore alizaliwa mwaka 1962 na  Demetria Gene Guynes katika eneo la  Roswell, New Mexico. Baba mzazi wa Demi aliachana na mama yake miezi michache kabla hajazaliwa. Mama aliolewa na mwanamume mwingine wakati Demi akiwa na umri wa miezi mitatu. Familia yao ilikuwa ikiishi katika eneo la watu wasiojiweza na mama na baba yake wa kambo walikuwa ni walevi. Kutokana na hali hiyo, familia yao ilikuwa ni ya vurugu na uhusiano usioeleweka.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Demi kuachana na shule na kutengana na familia yao akiwa na umri wa miaka 16 kwa lengo la kuendeleza kazi yake ya uanamitindo. Akiwa na umri wa miaka 17, Moore aliamua kujitosa kwenye darasa la uigizaji. Bada ya kuhitimu masomo yake, mwaka 1984 aliweza kushiriki katika filamu ya  Blame It on Rio  na  St. Elmo’s Fire  iliyotengenezwa mwaka  1985.
Hata hivyo, nafasi aliyocheza  mwaka  1986  katika filamu ya  About Last Night ndiyo iliyomfanya  Demi Moore  kuwa nyota katika kijiji cha  Hollywood. Pamoja na kupitia katika mazingira hayo, mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 53 anakadiriwa kuwa na utajiri unaozidi dola milioni 150.
  1. Shania Twain
shania-twain-picture-5Mama mzazi wa Shania Twain anaitwa Eileen Regina Edwards na alimzaa mwaka 1965 katika eneo la Windsor, Ontario.
Wazazi wake walitengana akiwa na umri wa miaka miwili na hivyo mama akaamua kuchukua mwanawe na kwenda  kuishi naye katika eneo la  Timmins, Ontario.
Hata hivyo, hakuchukua muda  mrefu kwa mama yake  Shania kuolewa tena.
Pamoja na kuolewa, familia yao ilikuwa ya kimasikini na mara nyingi walikuwawakishindwa hata kupata chakula cha kuwatosha. Wakiwa naishi katika maeneo ya vijijini, Shania alijifunza jinsi ya kuwinda na kukusanya kuni.
Mbali na hilo, mama na baba yake wa kufikia  walikuwa wakigombana mara kwa mara,  hali ambayo ilisababisha mwaka 1979 mama yake kumchukua mwanawe na kwenda kuishi naye kwenye  nyumba za watu wasio na makazi katika mji wa Toronto, wakati baba yake wa kufikia akiwa kazini.
Hata hivyo, familia hizo zilikuja kuungana tena mwaka 1981 na  Shania akajitosa katika fani ya muziki  na utunzi wa nyimbo kwa ajili ya kutatua  matatizo ya familia yao na kuondokana na umasikini. Akiwa na umri wa miaka 21, mama mzazi na baba wa kambo wa  Shania walikufa kwenye ajali ya gari. Kutokana na tukio hilo ikamlazimu Shania kuweka kando ndoto zake za kuwa mwimbaji ili aweze kuwatunza  ndugu zake wadogo. Baada ya kuhakikisha wana uwezo wa kujitunza, Shania  alitimkia mjini mji wa Nashville na albamu yake binafsi ya  ‘Shania Twain’ aliifyatua mwaka  1993. Baada ya kupitia katika mazingira hayo magumu, mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 50 utajiri wake kwa sasa unakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola milioni 350.
  1. Leighton Meester
Leighton Meester ambaye aliigiza kama Blair Waldorf katika filamu ya Gossip Girl ana utajiri tofauti na alipotokea.
Staa huyo alizaliwa mwaka 1986  katika eneo la  Fort Worth, Texas. Mama yake mzazi  Leighton alikuwa akitumikia kifungo gerezani kwa biashara za dawa za kulevya  wakati akizaliwa.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu mama yake Meester aachiwe ili akamtunze kwa muda wa miezi mitatu na nusu na kisha arejee gerezani akamalizie kifungo chake kilichokuwa kimebaki.
Hali hiyo ilimfanya Leighton akalelewe na bibi yake katika kisiwa cha Marco  kilichopo   Florida, kabla ya mama yake kuachiwa kutoka gerezani wakati Leighton akiwa na umri wa miaka  11.
Baada  ya kuachiwa, wawili hao walihamia jijini  New York  na  Meester akaanza kazi ya uanamitindo. Mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 14, yeye na mama yake walihamia  jijini Los Angeles, ambapo Leighton alipata shavu wakati alipopewa fursa ya kuigiza kama  Blair Waldorf katika filamu ya Gossip Girl.
Kwa sasa Leighton Meester anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 5.
.J.K. Rowling
J.K. Rowling  mama yake anaitwa  Joanne Rowling na alijikuta akilelewa na mama yake  wakiishi katika nyumba za umma nchini Uingereza na wakati akiandika maelezo yake ya kwanza wakati akiomba makazi ya umma, Mama yake Rowling aliandika kwamba “Yeye ni masikini  hana nyumba.”
Mama huyo aliandika maombi hayo kwa mkono huku mwanawe akiwa  pembeni kutokana na kuwa hakuwa na uwezo wa kumudu kutumia mashine ya kuandikia. Kutokana na hali hiyo katika mahojiano  na  gazeti la Daily Mail, mama yake Rowling anakumbuka kuwa hakuwa na uwezo wa kupata chakula, bali kitu pekee alichokuwa akikiweza ni kumlisha mwanawe.
Kwa sasa  J.K. Rowling anakadiriwa kuwa na utajiri unaozidi dola bilioni 1.
  1. Oprah Winfrey
oprah-winfrey-Nidaa 
Kabla  ya kuwa mahiri kwa sasa, Oprah Winfrey alikuwa binti masikini aliyekulia katika kijiji kidogo cha mashamba ya nguruwe kilichopo eneo la Kosciusko, Mississippi.
Winfrey alizaliwa na vijana ambao hawakuoana na alilelewa na bibi yake hadi alipofikisha umri wa miaka sita wakati yeye na mama yake walipohamia  Milwaukee, WI.
Mama yake alikuwa ni mhudumu ambaye alikuwa akifanya kazi muda mrefu bila kusaidiwa wala kuhurumiwa. Akiwa na umri wa miaka 14, Oprah alipelekwa akaishi na baba yake mjini Tennessee. Licha ya kuwepo na sheria ngumu kuhusu maadili ya kazi yake lakini alisaidiwa na  elimu yake. Wakati akiwa mdogo, Oprah alikuwa akivaa nguo za magunia ya viazi ingawa kwa sasa anavaa za kubuni.
Akiwa na utajiri ambao unakadiriwa kuwa  zaidi ya dola bilioni 2.9, Oprah Winfrey anasadikika kuwa ndiye anayeongoza kwa utajiri kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika.

No comments