• Latest News

  April 23, 2016

  Warembo 14 wajitosha Miss Tabata 2016


  WAREMBO 14 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka malkia wa Tabata mwaka huu ‘Miss Tabata 2016’imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
  Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi kila siku kwenye Ukumbi wa Da West Park, ulioko Tabata jijini.

  Aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Latifa Dibwe (18), Salma Abeid (18), Fatma Mapunda (19), Dinnah David (22) na Joyce Kweka (24).

  Wengine ni Neema Makwaia (22), Jesca Daniel (22), Sabrina Kipunga (22) Happiness Mnyeke (20), Grace Matiko (20), Olanda Filima (19),Neema Zablon (21),Joyce Nyimbo (24) na Noela Kyombya (24).

  Naye Mkurugenzi wa shindano hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kambi, Godfrey Kalinga alisema warembo hao wanafundishwa na Neema Mchaki, mkufunzi wa zamani wa shindano la Miss Ilala na Miss Tanzania 2014.

  Kalinga aliwaomba warembo wengine wenye sifa kujitokeza kushiriki kwenye shindano hilo, ambalo huvutia wadau wengi wa sanaa ya urembo nchini.

  “Bado tunapokea warembo, tunataka kufanya shindano la kihistoria mwaka huu na tumepanga kuwapeleka washiriki kwenye mbuga za wanyama ili kupromoti utalii wa ndani,” alisema Kalinga.

  Aliongeza kuwa washiriki watano watakaoshika nafasi za juu katika shindano hilo wataiwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Kanda ya Ilala ‘Miss Ilala’ na baadaye Miss Tanzania.

  Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment wakati Ambasia Mallya ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.

  Alizitaja kampuni zilizothibitisha kudhamini Miss Tabata kuwa ni CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 na Bob Entertainment.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Warembo 14 wajitosha Miss Tabata 2016 Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top