Header Ads

Wastara amshikia kisu mbunge...Mkasa mzima upo hapa


Wastara Juma

Dar es Salaam: Untold story! Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ambaye hivi karibuni ndoa yake na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliingia kwenye mgogoro mkubwa, alijikuta akimshikia kisu mumewe huyo, kitendo ambacho kilimtisha jamaa huyo ambaye hakutarajia kama mwanamke anaweza kumfanyia hivyo.

NI SIMULIZI YA KUSHANGAZA
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimenyetisha simulizi hiyo ya kushangaza ambapo kilidai kwamba, Wastara si mwanamke wa kumchezea ndiyo sababu kubwa iliyomfanya mbunge huyo kunyoosha mikono na kumuacha aende zake.
Kilisema kuwa, wakiwa katikati ya ugomvi wao wa kindoa, Sadifa alishtushwa na kitendo cha Wastara kumshikia kisu, jambo ambalo lilikuwa ni mapema mno akipiga hesabu za huko mbele itakuwaje?
MAMBO MENGI
Chanzo hicho kilitiririka kwamba, katika ndoa hiyo iliyodumu kwa muda wa takriban miezi mitatu, kulikuwa na mambo mengi nyuma ya pazia na kushukuru kuwa bora hata imevunjika kwani kati yao huenda kungetokea jambo kubwa zaidi, aidha mmoja wao kumwaga damu au hata kuaga dunia kwani kila mmoja alikuwa akijihami kwa jinsi anavyojua namna ya kutumia silaha kali.
WASTARA AMSHIKIA KISU
“Siku ya mwisho hadi Wastara akaamua kuondoka kwenye ndoa yake, mheshimiwa alitaka kumpiga ndipo Wastara akaamua kumshikia kisu kwa madai kuwa yeye huwa hapigwi, kiufupi wale wasingewezana,” kilidai chanzo.Sadifaaaaaaaa
Sadifa Juma
WASTARA ABANWA
Baada ya madai hayo mazito na ya kushtua, mwanahabari wetu alimwendea hewani Wastara na kumbana kuhusiana na habari hiyo ambapo mwanamama huyo alifunguka mazito zaidi.
Ijumaa: Wastara kwanza pole na kuvunjika kwa ndoa yako, hivi ni kweli uliwahi kumshikia kisu mbunge kwenye mgogoro wenu wa ndoa?
Wastara: Dah! Nimechoshwa na hizi habari jamani kwa sababu
zinanisononesha sana kwani nimekuwa mimi ndiye naonekana muovu.
MAOVU MENGI
Kuna maovu mengi ya mbunge ambayo sasa nitayaweka wazi. Niliyaacha kwa sababu ya kumheshimu kama mume wangu lakini yeye alifunguka, naomba muandike yote msifiche.
Hiyo habari ni ya ukweli wala hamjakosea, nilimshikia kisu kwa sababu nilikuwa nikijihami. Katika maisha yangu kupigwa ni mwiko, yeye alijaribu kunipiga na mimi nikamshikia kisu kwa kujihami.
Ijumaa: Huoni kama ni kosa kubwa na ulihatarisha maisha yake?
WASTARA KISU, MBUNGE PANGA
Wastara: Niliamua kumshikia kisu kwa sababu kubwa ya msingi ambayo ni baada ya yeye kunishikia panga, hiyo ni kawaida yake kwani hata ndani kwake ana mapanga mawili ambayo ameyahifadhi chini ya kitanda.
Ijumaa: Kuna madai kuwa uliondoka nyumbani kwake na kufungasha kila kitu alichokununulia kama aseti, unalizungumziaje hilo?
Wastara: Kweli nilibeba kila kitu lakini hakuna chake hata kimoja.
NINI KISA NA MKASA?
Ijumaa: Nini hasa sababu ya kuachana na mumeo maana hujawahi kufunguka kama hivi?
Wastara: Ni mambo mengi na wakati naolewa naye sikuyajua, nilianza kuyaona kwenye mitandao ya kijamii siku chache baada ya ndoa. Watu walikuwa wakinionea huruma, mimi sukujua lakini baadaye ndipo nilipoyaona yote.
WASTARA NA WANAUME
Ijumaa: Kuna madai kuwa una mpango wa kurudi kwa Bond ndiyo sababu ya yote hayo je, kuna ukweli juu ya hilo maana hata michango hamjarudisha kwa sababu mtafanya harusi nyingine?
Wastara:  Hakuna ukweli, mimi sina hamu na wanaume tena. Bond naongea naye kwa sababu alinithamini na kuujua utu wangu kwa kukiri makosa aliyonitendea. Kuhusu michango hakuna msanii hata mmoja aliyetoa zaidi ya ndugu zangu.
WASTARA ATOA NENO ZITO
Ijumaa: Je, mumeo akikufuata urudi myamalize, uko tayari?
Wastara: Siwezi kurudi kwa yule mbunge. Sikuwahi kumpenda wala yeye hakuwahi kunipenda, nilijikuta tu nimeshaingia kwenye ndoa.
Ijumaa: Kwa nini unasema hajawahi kukupenda?
Wastara: Kwa sababu alikuwa akinitukana. Kiufupi alininyanyasa, mbali na hapo hakuwahi kuwapenda hata watoto wangu.
SADIFA VIPI?
Baada ya Wastara kufunguka mazito, mwandishi wetu alimtafuta Sadifa lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS  hakujibu.
Hata hivyo, Hivi karibuni Sadifa alitoa ufafanuzi wa ndoa yake na kuanika baadhi ya mambo kwenye magazeti yaliyopita kuwa Wastara alikuwa akimwendea kwa waganga na kuahidi kumpa talaka.
USIKAE MBALI NA MAGAZETI
Ijumaa lina mambo mengine mazito ambayo yanahitaji mbunge kufunguka iwapo atapatikana na kujibu tuhuma hizo tutawaletea mwendelezo wa habari hii.
CHANZO: GPL

No comments