Header Ads

Wastara atolewa mahali ya shilingi milioni 5 na JUMA Mbega


DAR ES SALAAM: Bahati! Siku chache baada ya nyota wa sinema za Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kumwagwa na aliyekuwa mume wake, Sadifa Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge kwa Chama Cha Mapinduzi, kuna habari kuwa, mtalikiwa huyo ametolewa mahari kiasi kikitajwa kuwa ni shilingi milioni 5, Amani limehabarishwa. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Juma Mbega ambaye ni mcheza filamu na mfanyabiashara wa jijini Dar, anataka kumuoa Wastara baada ya kumuona anateseka tangu kifo cha aliyekuwa mume wake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’. 


TWENDE NA CHANZO “Nyie mnaandika, Wastara ameachwa na Sadifa, lakini mnajua kuhusu kutolewa mahari? “Kuna bwa’mdogo mmoja anaitwa Juma Mbega. Ni mfanyabiashara, amejitokeza kumuoa Wastara na ameshatoa mahari ya shilingi milioni tano. Fuatilieni wenyewe, mimi huo ndiyo ubuyu wangu,” kilisema chanzo hicho.

 AMANI LAMSAKA MUOAJI

 Baada ya kubebeshwa habari hizo, Amani lilimtafuta Juma na kuzungumza naye kwa njia ya simu ambapo alikiri kutoa kiasi hicho cha pesa kwa Wastara. “Nimempa shilingi milioni
tano, mshenga wangu, anaitwa Hamis Ramadhan. Zinakwenda kwa Wastara. Kusema kweli nataka kutuliza tabu zake. “Namjua Wastara tangu enzi za Sajuki. Kwa vile ameshaachika na yule mbunge, mimi nachukua nafasi yake.”

 HUYU HAPA MSHENGA 

Pia Amani lilizungumza na mshenga huyo ambapo alisema, Aprili 18, mwaka huu, Juma alimpa kiasi hicho cha pesa kupeleka kwa akina Wastara. “Ni kweli Juma alinipa hizo pesa Jumatatu. Lakini nilikosa nafasi ya kuzipeleka kwa Wastara kule kwao. Ila leo (juzi Jumanne) nitazipeleka. Yangu ni hayo tu,” alisema mshenga huyo. 

WASTARA SASA 
Baada ya kuzungumza na wote hao, Amani likamvutia ‘waya’ Wastara na yafuatayo ndiyo maneno yake na gazeti hili. “Huyo Juma namfahamu, jana (ana maana Jumatatu) nilikutana naye, akaniambia. Siwezi kusema mengi nasubiri. Alisema nusu ya hizo pesa nimrudishie mahari yake Sadifa, mimi sirudishi hata senti tano kwani yeye si alinitumia kama mwanamke!”  Amani: “Kwa hiyo wewe Wastara uko tayari kuolewa tena?” Wastara: “Hata mara kumi naweza kuolewa kwa sababu mimi ni mtoto wa Kiislamu hilo kwangu linakubalika bila shida.” Wastara aliongeza kuwa, inapotokea ameachana na mtu ni kutokana na mwanaume kushindwa kutimiza vitu muhimuambavyo mwanamke anatakiwa kuvipata kwa mume wake.

SHERIA ZA KIISLAMU
Kwa sheria za Kiislamu, Wastara ni huru kuolewa baada ya kupewa talaka tatu ambapo kwa mujibu wake, Sadifa hajampa talaka rasmi hivyo kuwa na ugumu ikisemekana ndugu wa Wastara wanahaha kuipata talaka hiyo.

 KWA NINI JUMA... JUMA...JUMA? Kama Wastara atafikia kiwango cha ndoa na mtu huyo, atakuwa ameingia kwenye ndoa na Juma tena hali inayoibua maswali. Marehemu Sajuki aliitwa JUMA Kilowoko, mbunge anaitwa Sadifa JUMA, huyu wa sasa ni JUMA Mbega huku yeye mwenyewe akiitwa Wastara JUMA.

 MAISHA YAKE YA NDOA
Wastara amepitia katika maisha ya uhusaino na ndoa kwa wanaume kadhaa. Mwaka 2000 alifunga ndoa na Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kumwagana wakiwa wamezaa mtoto mmoja, Fares. Mwaka 2009, Wastara alifunga ndoa na msanii wa filamu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mwaka, 2013. Walibahatika kuzaa naye mtoto mmoja, Farheen. Mwaka 2016, akafunga ndoa na Mbunge Sadifa lakini mwaka huu walimwagana na sasa anatarajia kuingia kwenye ndoa nyingine.

CREDIT: AMANI GAZETI

No comments