Header Ads

Zigo ni moja ya sifa za Video Queen Bongo?


Kwenye ulimwengu wa burudani, mwanamuziki anapotoa wimbo wake, kinachofuata ni kuutengenezea kideo au wengine huita kichupa! Huo ndiyo utaratibu uliopo kwa wasanii wengi licha ya baadhi yao kutambaa na audio mwanzo mwisho! Wasanii ambao hutoa audio bila kuzitengezea video, sababu kubwa ni kukosa mkwanja. Bila kuwa na pesa ya kutosha huwezi kutengeneza video ambayo inaweza kukupaisha. Ndiyo maana wapo ambao wana nyimbo nzuri tu lakini mpaka leo hawajazifanyia video.

Unapozungumzia ishu ya kuandaa video, wapo watu wanaoitwa video queens. Hawa ni wale wadada wanaotumiwa
kuifanya video husika itazamike na ndiyo maana wengi wanaotumika wanavutia kinomanoma! u-video queen umekuwa ni dili kwa wasichana wengi Bongo, baadhi wameigeuza kuwa ni kazi ya kuwapatia kipato kinachowapa jeuri ya kutamba mjini. Niliwahi kumuuliza mmoja wa wasanii wanaokuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa muziki Bongo anayefahamika kwa jina la Starick sababu ya kutumia warembo kwenye
video ya wimbo wake uitwao Nipe Wakaseme. Nikamuuliza ni kwa nini wanamuziki wengi huwatumia wasichana waliofungashia kwenye video zao, akasema: “Unajua unapoandaa video lazima utumie watu ambao watamshawishi mtu awatazame, iwe wanapocheza, wakiwa wanatembea au hata wakiwa wamepozi. “Ndiyo maana wanaokula shavu la kwenye video wengi wao wana figa bomba. Hata yule niliyemtumia kwenye wimbo wangu wa Nipe Wakaseme (Naima), si unaona alivyo bomba?”
ZIGO NI MOJA YA SIFA? Licha ya maneno ya msanii huyo, uchunguzi niliofanya unaonesha kuwa, wasichana wanaotumika kwenye video za wanamuziki licha ya kwamba wanatakiwa wawe na sifa nyingine, kufungashia kunaweza kuwabeba pia. Wacheki akinadada kama Masogange, Gigy Money, Kidoa na Lulu Ladiva. Hawa ni kati ya wasichana wanaotesa kwenye video nyingi. Wamejaaliwa maumbile f’lani ‘amazing’ kiasi cha kuwafanya wapate dili za kuonekana kwenye vichupa vingi tena kwa mkwanja mnono. Kwa bahati nzuri wasichana hao niliwahi kuongea nao kwa nyakati tofauti kuhusiana na kazi hiyo. Wengi walionekana kumshukuru Mungu kwa kuwaumba hivyo walivyo wakidai kuwa maumbile yao yanawafanya wapate madili kibao ukiachilia mbali
hilo la kuonekana kwenye vichupa. “Najivunia sana shepu yangu, hii ndiyo inaniweka mjini. Nafanya muziki, napata madili ya matangazo lakini pia kuonekana kwangu kwenye events ni pesa. Kwa nini nisimshukuru Mungu kwa kuniumba hivi nilivyo?” alihoji Gigy.
KUNA SIFA NYINGINE Tunapozungumzia u-video queen, mbali na kuwa na umbile tata, lazima sura yako pia iwe na mvuto, uwe mcharuko kiaina na usiwe na aibu. Ukifuatilia mavideo queen wengi utaona kutupia picha mtandaoni zikiwaonesha wakiwa nusu watupu wala siyo ishu. Ni kama wamepinda f’lani hivi kiasi kwamba wengi wanahoji; hivi kuwa video queen lazima watu wakuone ulivyo? Video queen lazima uwe mcharuko na usiye na aibu? Maswali hayo majibu yake ni rahisi sana. Siyo kwamba kila video queen lazima awe mcharuko. Wapo mavideo queen ninaowajua ambao siyo mapepe, wanajiheshimu na siyo watu wa kujianika nusu utupu kila wakati. MCHINA ANAHUSIKA! Baada ya kuonekana kwamba wenye ‘mizigo’ wana soko sana, wapo baadhi ya mabinti ambao wanatajwa kutumia dawa za Kichina kukuza makalio yao huku wengine wakijaladia wanapokuwa lokesheni. Si ajabu ukakutana mtaani na video queen akiwa kafungashia ile mbaya lakini ukimuona akiwa anatoka kuamka utashangaa yuko flati. Hao ndiyo wale wanaojaladia kwa kuvaa taiti zilizowekewa masponji.
CREDIT: Ijumaa

No comments