Header Ads

A-Z Fumanizi la Shilole, Madee!


Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Stori: Gabriel Ng’osha na Sifael Paul
YAMEIBUKA tena? Ni takriban mwaka mmoja na ushee tangu skendo ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na staa mwenzake wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ kudaiwa kufumaniwa na aliyekuwa mpenzi wa Shilole, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambapo kila mtu alijitetea kwa upande wake.
 SHILOLENAMADEE2
Shilole na Madee
Lakini wikiendi iliyopita, Nuh aliibuka na kuifunua upya skendo hiyo ya kumfumania Shilole laivu akimsaliti na Madee wakiwa hotelini, jambo lililomuuma kila anapokumbuka tukio hilo. Kwa mujibu wa Nuh, aliwakuta wawili hao wakivunja amri ya sita huku mmoja wao akiwa mtupu kama alivyozaliwa.
shilole (2)Nuh alidai kuwa hapendi sana kuzungumzia suala lake la uhusiano wa kimapenzi kwani linawafanya watu kusahau muziki wake na kusikiliza mambo mengine nje ya kazi zake. Lakini kuhusu kumfumania Shilole na Madee hotelini walipokuwa kwenye shoo katika moja ya Mikoa ya Tanzania Bara (hakusema mkoa gani), Nuh alisema kuwa ni kati ya mambo yaliyokuwa yakimuumiza kabla ya kuachana na Shilole.
Kufuatia ishu hiyo kuibuliwa upya na Nuh ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipoachana na Shilole, imeibua mjadala mzito kwa baadhi ya mashabiki wa mastaa hao huku wengine wakidai inawezekana Nuh ameibua skendo hiyo kwa nia ya kupata kiki ya wimbo wake mpya wa Jike Shupa ambao inadaiwa kuwa amemuimba Shilole. Kufuatia kuibuka upya kwa skendo hiyo, Wikienda lilizungumza na Shilole na Madee juu ya fumanizi hilo.
Madee2
MADEE
Akijibu tuhuma hizo kupitia Global TV Online, Rais wa Manzese, Madee anayetamba na wimbo wake mpya wa Miguru Pande alikuwa na haya ya kusema:
“Kiukweli hata mimi nimesikia na nimeshangaa kuzuka kwa tuhuma hizo. “Mimi na Shilole ni marafiki wa muda mrefu sana hata kabla Nuh hajamfahamu Shishi (Shilole) na ninaamini wakati Nuh anaingia kwenye uhusiano na Shilole alijua mimi ni rafiki wa Shishi.
“Hicho anachokisema sasa inawezekana ni kutafuta ‘kiki’ maana siku hizi wasanii wakitaka kutoa wimbo au video wanatafuta cha kufanya ili wawe midomoni mwa mashabiki so labda anafanya hivyo ili apate kiki ya ngoma yake mpya.”
45245952fc8c5c5e099a3e444bf8f32a_XLSHILOLE
Kwa upande wake Shilole aliyeachia wimbo wake mpya wa Say My Name alipozungumza na Wikienda kwa njia ya simu alidai kuwa hawezi kumjibu mtu muongo.
“Alikuwa wapi kusema kabla hatujaachana? Mimi siwezi kuongea chochote kuhusu hilo labda anatafuta kiki. Mimi nina heshima zangu, kwanza hapa nipo wilayani Igunga (Tabora) kuna kazi nafanya,” alisema Shilole.
WASIKIE MASHABIKI WAO
Mara baada ya Nuh kuiibua upya skendo hiyo, Wikienda lilifanya mahojiano na baadhi ya mashabiki wa wasanii hao ambapo wengi wamesema Nuh hana lolote zaidi ya kupenda kurudiana na Shilole au kutafuta kiki tu.
“Kinachomsumbua Nuh ni maumivu ya kuachwa na Shilole, alikuwa wapi kusema hivyo wakati wa uhusiano wao?” alihoji shabiki wao aliyejitambulisha kwa jina la Zahra Juma.

No comments