Header Ads

Binti wa kwanza wa Obama, Malia mwenye miaka 17 kusomea HarvardMwanaye rais wa Marekani Barack Obama, Malia, amefuzu kujiunga na chuo kikuu cha Harvard.
Taarifa kutoka ikulu ya White House imesema kuwa Malia ambaye amekuwa mapumzikoni baada ya kuhitimu masomo ya chuo cha upili, atajiunga na chuo hicho cha kifahari mwakani.
 Sasha na Malia Obama.
Malia ataendelea na likizo yake kabla ya kujiunga na Harvard mwakani.'' taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.

Malia mwenye umri wa miaka 17 atakuwa anafuata nyayo za wazazi wake rais Obama na Mitchel ,ambao wote walihitimu na Shahada ya Sheria kutoka Kitivo cha Sheria cha chuo kikuu cha Harvard.

Chaguo lake la chuo kikuu limekuwa likijadiliwa haswa na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.

Malia ndiye binti wa kwanza wa rais Obama.
Binti mwengine wa rais huyo mwenye asili ya Kenya anaitwa Sasha na anaumri wa miaka 15.
 CHANZO: BBC SWAHILI

No comments