Header Ads

Video: Chid Benz Adaiwa Kutoroka Sober HouseMsanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.DAR ES SALAAM: Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa jamaa alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa. 

Chid

Taarifa iliyotua kwenye meza ya dawati hili ilidai kuwa, Chid alitoroka kituoni hapo baada ya kushindwa kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora arudi mtaani kwa staili ya liwalo na liwe.

Baada ya kupata taarifa hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita waandishi wetu walitinga Bagamoyo na kukutana na meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura ambaye alithibitisha kuondoka kwa Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu. Sehemu ya mahojiano kati ya Risasi na meneja huyo ni hii;

Chid-Beenz_fullRisasi: Kwani Chid Benz ameishi hapa kwa muda gani?

Tumaini: Ni siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida.

Risasi: Ilikuwaje sasa mpaka akaondoka kabla hajawa sawa?

Tumaini: Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa.

Risasi: Hali ilikuwaje kwa meneja wake wakati Chid anang’ang’ania juu ya jambo hilo?

Tumaini: Kiukweli hakuwa akitaka aondoke maana mara kwa mara alikuwa anamsihi kuwa mvumilivu ili amalize angalau miezi mitatu na ampeleke kwenye shoo za muziki ndani na nje ya nchi, lakini Chid hakujali hayo. Kwa hiyo siwezi kusema alifurahia juu ya jambo hilo.

Risasi: Maisha yake ya kawaida yalikuwaje na wenzake?

Tumaini: Hayakuwa mabaya sana japo alikuwa mzito kushiriki kwenye ishu za usafi na vitu vingine. Muda mwingi alipenda kupumzika na kuandika mistari. Lakini kuna kipindi alikuwa akijaribu kuhamasisha wenzake wagomee kitu fulani. Sisi tulikuwa tunamchukulia kama mtu wa kawaida aliyekuwa anahitaji msaada kutoka kwa viongozi.

Baada ya mahojiano hayo, waandishi wetu waliamua kumtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.

Alipopatikana, Babu Tale alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chid, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”

CHANZO: Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata, RISASI

No comments