Header Ads

Chombezo: Baba’ke Mdogo Kaka - 03


ILIPOISHIA RISASI JUMATANO: “Sawa...sasa je, kwa mfano... nikisema nimeshaachana na mama yako halafu sasa nikakuomba wewe kwa vile ni msichana wa rika langu, uwe mpenzi wangu utanikubalia?”

 JIACHIE MWENYEWE SASA...
LIANA aliachia tabasamu kwa mbali kisha akamwangalia Chidi kwa jicho la kumshangaa kwa swali lake. Akabaini kuwa, alianzia mbali mpaka kumwingiza kwenye mkenge wa swali hilo, akarejea na mazungumzo yenyewe... “Sasa mfano sasa, nikisema sawa mimi na mama yako tunaachana, utafurahi wewe Liana?” “Sana, tena naweza kufanya sherehe kuliko hii aibu mnayotupa...

” “Sawa...sasa je, kwa mfano... nikisema nimeshaachana na mama yako halafu sasa nikakuomba wewe kwa vile ni msichana wa rika langu, uwe mpenzi wangu utanikubalia?” “Hivi kwa nini umeniuliza hivyo?” Liana alimuuliza Chidi akiendelea kutabasamu... “Nimekuuliza kwa sababu umesema kwa nini nisitafute msichana wa rika langu wakati wapo tele kuliko kuwapa aibu kwa kuwa na mama yenu... “Lakini mimi nilipokuona tu nilijua wewe ni msichana wa rika langu lakini sasa ni mwanangu na hutaki uwe mwanangu...” “Kwangu imeshakuwa ngumu maana upo na mama...” “Si umesema niachane naye kuliko kuwapa aibu?” “Ndiyo...” “Sasa naomba niwe na wewe basi...” “Ina maana ukiwa na mimi ndiyo utaachana na mama yangu?” aliuliza Liana huku akiachia tabasamu laini lililoufanya uso wake uonekane kama ametoka saluni muda huohuo...

 “Yeah! Tena naamini wewe ndiyo utakuwa msaada mkubwa sana wa mimi na mama yako kuachana,” alisema Chidi huku akichomoa kutoka kwenye mfuko wa suruali, simu yake ya kisasa na kubonyezabonyeza... “Nitakusaidiaje sasa wakati tayari uko na mama yangu?” alisema Liana... “Kha! Liana, unakijua unachokisema?” aliuliza Chidi... “Nakijua sana...” “Kwamba..?” “Kwamba achana na mama yetu, tafuta msichana mwingine wa rika lako...” “Naomba uwe wewe Liana!” “Mimi ngumu kwa sababu...” “Kwa sababu si wa rika langu?” alidakia Chidi... “Hapana, ila tayari upo na mama...” “Si unasema niachane naye!” “Oke...achana naye...” “Kwa hiyo upo tayari wewe uwe na mimi?” Kabla Liana hajajibu, gari lilifika getini, alikuwa mama yake, akapiga honi. Liana alitoka mbio sebuleni, akaenda kufungua geti, mama yake akaingia mpaka ndani, akashuka... “Baba yako amerudi?” “Amerudi, shikamoo mama...”

“Marhaba, amekula chakula?” “Bado...” “Kwa nini?” “Ameingia muda huuhuu ...sawasawa na wewe.” “Kaandae chakula haraka sana,” mama Liana alisema kwa amri. *** Liana alikuwa jikoni akiandaa chakula, akamuwaza mama yake, akamuwaza Chidi... “Lakini ni kijana mzuri sana, mtanashati tena. Ana mwili mzuri, hata rangi yake nzuri ila amekosea kuwa na mama mtu mzima kama mama yangu...kwa nini lakini? Mama amemdanganyaje yule kaka?” alijiuliza sana Liana huku akiendelea na mapishi. Kwa upande wake, Chidi aliamini kuwa, kama Liana akimkubalia atakachofanya ni kula kuku na mayai yake... “Hakuna namna, maana mtoto mzuri kweli, kaumbika kila idara lakini mama naye ni msaada mkubwa kwangu, siwezi kumuoa ila nashikamana naye kwa sababu ya pesa,” alijisemea moyoni Chidi. *** Liana alitenga chakula, akamfuata Chidi mpaka jirani akapiga magoti na kusema...

“Baba chakula tayari...” “Sawasawa Liana,” alisema mama yake kwa vile binti yake alivyomwita Chidi baba bila shuruti. “Haya asante sana Liana,” alisema Chidi huku akisimama na kwenda kwenye meza ya chakula. Liana alimnawisha maji Chidi, wakatazamana kiaina, Liana akaachia tabasamu na kuondoka. Wakati Chidi akila, Liana alikwenda sebuleni na kukaa na mama yake... “Ngoja nikaoge kwanza na mimi nijue nini kinafuata kati ya kula au kulala kidogo maana nimechoka sana,” alisema mama Liana akisimama kwenda chumbani kwake kuoga.

 Liana alimwangalia Chidi, akamwona amezama kwenye mlo, akamfuata... “Sasa wewe baba ulikuwa unatakaje kwani?” aliuliza Liana huku akiangalia nyuma kwa tahadhari. “Mimi nataka niwe na wewe...” “Halafu mama?” “Si ndiyo basi...au we unasemaje?” “Mh! Ngoja nakuja kukujibu,” alisema Liana akiondoka. Alikwenda mpaka chumbani kwa mama yake kwani alikuwa akiingia anavyotaka. Alipobaini mama yake ameshaingia bafuni kuoga, alitoka haraka mpaka kwa Chidi... “Enhe...sasa mama akijua wewe uko na mimi unadhani itakuwaje?” Liana alimuuliza Chidi... “Utamwambia?” “Aka! Mi siwezi kumwambia...” “Sasa unadhani atajuaje?” “Mh! Kama nahofia fulani, unajua huyu ni mama yangu sasa aje ajue wewe na mimi ni wapenzi, itakuwa balaa tupu!” “Kwani Liana, mimi naomba nikuulize swali moja dogo sana,” alisema Chidi... “Uliza...” “Unahisi mimi sina akili?” “Noo! Najua unazo sana...” “Basi amini mama yako hatajua hata siku moja katika maisha yake...” “Kweli baba?” “Kweli Liana.” Liana akaachia tabasamu laini na zuri, Chidi akaendelea... “Upo tayari Liana?” “Yes baba, nipo tayari...” “Njoo nikaribie mpaka hapa,” Chidi alimwita Liana.
ITAENDELEA WIKI IJAYO JUMATANO

No comments