• Latest News

  May 17, 2016

  David Kafulila ashindwa kesi yake dhidi ya Hasna Mwilima mahakama kuu kanda ya Tabora


  Mbunge wa zamani wa   Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI), David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima
   
  Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuendeshwa  chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
   
  Katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: David Kafulila ashindwa kesi yake dhidi ya Hasna Mwilima mahakama kuu kanda ya Tabora Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top