Header Ads

Davina: Filamu za mapenzi wanazocheza wasanii wengi zimeua soko Bongo

 
MUIGIZA wa long time Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameibuka na kueleza kwamba filamu za mapenzi wanazocheza wasanii
wengi zimeua soko ndiyo maana kwa sasa ni kama sanaa hiyo haipo. Akichonga na paparazi wetu hivi karibuni, Davina alisema
kutokana na soko la filamu kuwa gumu wasanii wengi wameamua kugeukia biashara kwani wakikaa na kusubiria sanaa
hiyo watakufa njaa. “Tunapigana ili tulirudishe soko la filamu liwe kama zamani maana limekufa kutokana na filamu za
mapenzi tunazocheza mara kwa mara. Kuna kila sababu ya kubadilika kama kweli tunataka kulishika soko,” alisema Davina.

No comments