Header Ads

Diamond, Kiba pasu kwa pasu, mashabiki wao meno nje!


Ali Kiba baada ya kusaini mkataba na Kampuni ya Sonny.
HUKU mashabiki wa Ali Saleh Kiba wakifurahia mafanikio ya msanii huyo kutokana na kulamba shavu la kusaini mkataba na kampuni ya kimataifa ya Sony Music pamoja na kupewa ‘coverage’ na jarida maarufu la Marekani la The Source, mashabiki wa Diamond Platnumz nao meno nje!
diamondnaneyo 
Diamond na Ne-Yo
Hiyo imefuatia baada ya Diamond naye kutangazwa hivi karibuni kuwania Tuzo za Black Entertainment Television (BET 2016) kwa mara ya pili mfululizo akiwa katika Kipendele cha Best International Act: Africa, akichuana na wakali  wengine wakiwemo Wizkid, Yemi Alade (Nigeria), AKA, Cassper Nyovest na Black Koffie wote wa Afrika Kusini.
Mafanikio ya mastaa hao yanawapa nguvu wasanii wengi wanaochipukia na waliopo kwenye gemu kuamini kuwa inawezekana.

No comments