Header Ads

Gardner ajutia kumtusi Jide


SIKU chache baada ya kipande cha video kuonekana katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha mtangazaji maarufu, Gardner G Habash akitoa maneno ya matusi kwa mkewe wa zamani, Judith Wambura ‘Jide’, ameonekana kujutia kitendo chake hicho. Katika eneo ambalo linalotajwa kuwa ni katika Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Ijumaa ya wiki iliyopita, Gardner,
aliyejitambulisha kuwa ni Mtangazaji wa Clouds FM, alitoa maneno ya kidhalilishaji kwa msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya, baada ya kuulizwa na mashabiki kama alikuwa na matatizo na mtalaka wake. “Mimi sina neno na yule mtoto wa kike, nime… (tusi) kwa miaka 15,” alisema mtangazaji huyo, ambaye aliishi katika maisha ya ndoa na Jide kwa zaidi ya miaka kumi, kabla ya kutengana miaka miwili iliyopita Akizungumza na Risasi Mchanganyiko lililotaka kufahamu kisa na mkasa wa kutoa maneno hayo, Gardner alishindwa kuongea akidai alikuwa katika kikao, lakini alituma ujumbe mfupi wa maneno akisema;

 Gardner, aliyejitambulisha kuwa ni Mtangazaji wa Clouds FM.

“Kaka pole kwa usumbufu, sitakuwa na cha kusema kwa sasa ili kuepusha tafsiri isiyo sahihi, naomba nielewe mkuu. Asante.” Gazeti hili pia lilimtafuta kupitia simu yake ya mkononi mwimbaji huyo wa kibao cha Ndi Ndi Ndi, Jide lakini hakupokea.

 Hata Meneja wake, Severin Mosha maarufu kama Seven, alipoulizwa kama wana taarifa na kipande hicho cha video na mpango wao kuhusiana na jambo hili, alisema wameiona lakini hawana la kusema kwa sasa. Katika hali nyingine, Naibu Waziri wa  Afya, Jinsia na Watoto, Dk. Khamis Kigwangalla amekitaka Kituo cha Redio cha Clouds na Gardner kumuomba radhi Jide.

Chanzo: Risasi Jumatano/GPL
...

No comments