Header Ads

Hii ni list ya wanaume waliofaidi penzi la Jackline Wolper wakitumia mbinu ya kumvisha pete


Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta mtu sahihi wa kuwa naye maishani yaani mke au mume.
Staa wa filamu  za Kibongo, Jacqueline Wolper anaweza kuthibitisha hilo kwani pengine anaweza kuwa staa mwenye listi ndefu ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka na  mitini japo haikatishi ndoto zake za kumpata mtu sahihi wa kuwa nae kwenye mahusiano.
wolper gambeee 002Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha  kwa wazazi wao,lakini baada ya kufaidi penzi la mrembo huyu things fall apart na kupelekea mrembo huyu kuingia kwenye mahusiano mengine,hali iliyopelekea mashabiki wa muigizaji huyu kuhoji kwanini amekua akiangukia mikonononi mwa matapeli wa mapenzi na wengine wakienda mbali na kudai kuwa pengine mrembo huyu amekua akipenda fedha na sio mapenzi ya kweli kutoka wanaume aliokua nao hapo awali.
ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ na alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya uchumba na kumtambulisha mpaka kwa wazazi wake naye kujitambulisha kwa wazazi wa mwanadada huyo lakini walimwagana baada ya Wolper kuhisi kwamba anasalitiwa kwa mpenzi wake huyo kuwa na uhusiano na wasanii wenzake.

wolper gambeeee 001Dallas alikuwa akimpa Wolper fedha za kutosha ambapo kipindi hicho aliweza kumchangia msanii mwenzake ambaye ni marehemu kwa sasa, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kiasi cha Sh. milioni 15 kwa ajili ya matibabu nchini India huku katika kumbi mbalimbali za starehe akiwatunza wasanii wenzake vitita vya noti kama hana akili nzuri.
GEE MODO
Jamaa huyo ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya viatu na nguo maeneo ya Kinondoni jijini Dar ambapo baada ya Wolper kuachana na Dallas naye aliingia kwa gia ya kumvisha pete ya uchumba na mapenzi kuwa motomoto kwa kile kilichoonekana kwamba anampooza machungu.

Hawakukaa muda mrefu, wawili hao waliachana japokuwa sababu za kumwagana kwao hazikujulikana ila tayari jamaa huyo alikuwa ameshamfaidi penzi la mrembo huyu.
JIMMY MGAYA
Jimmy ni Mbongo aishiye Afrika Kusini ‘Sauz’ ambaye naye ni mfanyabiashara pia,Baada ya Wolper kuachana na Gee Modo alinasa kwa Jimmy ambapo kwa mara ya kwanza zilinaswa picha zao za kimahaba wakiwa nchini Afrika Kusini.

wolper gambe na jimy 004Hata hivyo, muda mfupi baada ya kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba, kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huo haukudumu kwa muda mrefu ukavunjika.
MWAMI RAJABU
Mwami ni mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara nyingi Mwami alionekana  jijini Dar es salaam kwa kazi zake za kibiashara ambapo hufikia hoteli za kifahari ambapo Mwami anatajwa kwamba aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wolper lakini hakuna kilichoendelea baada ya jamaa huyo kudaiwa kupata alichokitaka.

MKONGO
Katika kujaribu tena bahati yake, Wolper alijikuta mapenzini na Mkongo mmoja ambaye mpaka wanaachana jina lake halisi halikupatikana ambapo kama ilivyokuwa kwa wengine waliotangulia,mahusiano yao haukuchukua muda mrefu na walitengana.

wolper na mkongo 006 
Mkongo huyo alimvisha Wolper pete ya uchumba na alikuwa akisema mara kwa mara kuwa wapo kwenye mipango ya ndoa hata pale ukweli ulipogundulika kwamba ni mume wa mtu ambapo Wolper alidai hatasikiliza maneno ya watu,ila mwisho wa siku wakaja kumwagana baada ya Mkongo kumfaidi mrembo huyo.
MY TAKE :
Jackine Wolper kama muigizaji nnaeamini ana kipaji cha hali ya juu,ni wazi kuwa endapo akiwa kwenye mahusiano na mtu sahihi hata shughuli zake za kisanaa anaweza kuzifanya kwa ufanisi na kukata kiu ya mashabiki wake ambao wamechoshwa na drama za mgazetini na kwenye mitandao ya kijamii,hivyo kama kweli anaamini Harmonize ni mtu sahihi kwake huu ni muda muafaka wa kukaa chini na kutulia nae kwani licha ya wote wawili kuwa mastaa,ni wazi kuwa mahusiano yao yatakua na manufaa ya kibiashara kwenye kazi zao za kisanaa.
wolper and harmonizer 002

No comments