• Latest News

  May 08, 2016

  JULIO ANA MBWEMBWE JAMANI! SOMA UONE ANACHOWAAMBIA SIMBA  Kocha Mkuu wa MWadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ana kikosi bora kabisa ambacho hakiwezi kulinganishwa na kile cha Simba.

  Mwadui FC watakuwa wageni wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

  Julio anasema atashangazwa sana kama wao watapoteza mechi dhidi ya Simba hii leo.

  “Kweli mechi itakuwa na ushinda, huenda inaweza ikawa ngumu. Lakini nitashangazwa sana kama nitafungwa na Simba.


  “Nasema hivyo kwa kuwa nina kikosi bora kabisa ambacho huwezi ukakilinganisha na Simba. Tunachotakiwa ni kupambana na kushinda na hilo liko wazi,” alisema Julio aliyewahi kuwa beki wa kati wa Simba, kocha msaidizi na kocha mkuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JULIO ANA MBWEMBWE JAMANI! SOMA UONE ANACHOWAAMBIA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top