Header Ads

KABLA SIJAFA, DUNIA INISAMEHE - 6


Taarifa zilizorudi Uingereza kutoka Uganda miezi miwilibaada ya Johnson kurudishwa nyumbani ziliwasikitisha watu wengi, hakuna aliyekuwa tayari kuamini kuwa Johnson alikuwa amekufa kwa ugonjwa wa Ukimwi! Ugonjwa ambao haukujulikana chanzo chake na hakuna mtu yeyote aliyekuwa ameripotiwa kuugua katika nchi yote ya Uingereza.
Watu nchini Uingereza walianza kujiuliza maswali mengi kuhusu uhusiano uliokuwepo katika ya David Syndrome na Johnson na walianza kuhisi huenda tajiri David Syndrome pia alikuwa ameambukizwa baada ya taarifa kusambaa kuwa walikuwa na uhusiano wa kishoga.
Kifo cha Johnson kilikuwa pigo kubwa sana kwa wazazi wake waliokuwa na watoto wawili peke yake yaani Johnson na Dorothy waliokuwa mapacha, walishindwa kuelewa mtoto wao aliyeupata wapi ugonjwa huo hatari.
Siku tatu baada ya kufariki kwa Johnson, Dorothy aliwasili nchini Uganda kwa mazishi ya nduguye, afya yake iliwashangaza watu wengi kwani alikuwa amepungua kupita kiasi na nywele zilishaanza kunyonyoka kichwani kwake!
Vijana wengi wa umri wa Johnson na Dorothy nchini Uganda walikuwa wamefariki kwa ugonjwa wa Ukimwi na hakuna mtu hata mmoja nchini humo hata mawaziri waliokuwa wamehisi kuwa vifo hivyo vilitokana na chanjo ya polio iliyotolewa kwa watoto miaka zaidi ya kumi kabla! Na miongoni mwa watoto hao walikuwemo Dorothy na Johnson.
Kwa uzoefu waliokuwa wameupata watu wa Uganda baada ya kufiwa na vijana wengi waligundua kila dalili kuwa hata Dorothy pia alikuwa ameathirika! Hilo hata wazazi wake walipomwona walilihisi na walishindwa kuelewa ni wapi watoto wao wote waliupata ugonjwa huu hatari! Mioyo yao iliwauma sana kwani hawakuwa na uwezo wa kupata watoto wengine.

*****
Baada ya mazishi ya kaka yake Dorothy alirudi tena Uingereza ambako uhusiano wake wa kishoga na Suzanne uliendelea lakini hali yake ilizidi kuwa dhaifu siku hadi siku mwili wake ulizidi kupungua kila siku iliyokwenda kwa Mungu na uliota mapunye na ukurutu kila sehemu jambo lililomlazimisha kwenda hospitali kupimwa ili kujua tatizo lake.
Ni huko ndiko ilikogundulika kuwa naye pia alikuwa ameambukizwa virusi hatari vya Ukimwi! Na alikuwa katika hatua za mwisho kabisa za uhai wake, Dorothy alichanganyikiwa na alishindwa kuelewa ni kwanini yeye na kaka yake ndio wafe kwa ugonjwa ule.
Baada ya kupewa majibu hayo Dorothy hakumficha kitu Suzanne ilibidi amwambie kila kitu waziwazi, Suzanne alichanganyikiwa na kulia usiku kucha! Dorothy alishindwa kuelewa ni kwanini Suzanne alilia kiasi kile ikabidi amuulize.
“Suzanne why did you spend your last night crying?(Suzanne kwanini umekesha usiku kucha ukilia?)
“I’m sorry, so sorry Dorothy”(Samahani, samahani sana Dorothy)
“Sorry for what, baby?”(Samahani ya nini?)
“Sorry because I have killed you, your brother and many Ugandan Children and now I’m dying too”(Kwa sababu nimekuua, kaka yako na watoto wengi wa Uganda na sasa mimi mwenyewe ninakufa!)
“How did you kill me and my brother?”(Ulituua vipi mimi na kaka yangu?) Aliuliza Dorothy kwa mshangao.
“I guess you and Johnson were vaccinated with Polino vaccine in your country many years back, isn’t?”
“Ofcourse we were! It was a campaign that every child under five years in my home town was Vaccinated”
“Sure?”(Hakika?)
“Positively darling !”(Hakika mpenzi)
“I’m so sorry Dorothy, it was that time that I killed you and now it has come back to me!”(Samahani Dorothy ni wakati huo ndio niliwaua na sasa imerudi tena kwangu)
“What do you mean Suzanne?”(Unaamanisha nini kusema hivyo Suzanne?)
Badala ya kujibu swali Suzanne alijikuta akimwaga machozi na kuendelea kulia kwa muda mrefu huku Dorothy akimbembeleza na kumdadisi kwanini aliongea maneno yale magumu kueleweka, baada ya kumbana sana hatimaye Suzanne alijikuta akimsimulia Dorothy kila kitu kilichotokea na kumwomba msamaha.
“No! I can’t agree and cant forgive you because you have taken my life!”(Hapana siwezi kukubali na siwezi kukusamahe kwa sababu umechukua maisha yangu)
Suzanne aliendelea kulia huku akimweleza Dorothy jinsi walivyomtengeneza mdudu hatari wa Ukimwi, na kumtuma Uganda katika chanjo iliyotolewa kwa watoto laki tatu nchini humo.
“Suzanne why did you kill all our innocent souls?”(Suzanne kwanini uliua roho zetu zisizo na hatia?)
“Money! We wanted to be rich than Bill Gate Dorothy! Forgive me”(Pesa! Tulitaka kuwa matajiri kumpita Bill Gate Dorothy! Nisamehe sana)
“For money you kill 300,000 innocent peoples including me and my brother! What is the value of money as compared to human being’s soul?”(Kwa sababu ya pesa umeua watu laki tatu ambao hawana hatia yoyote nikiwemo mimi na kaka yangu! Nini thamani ya pesa na maisha ya watu?)
“I’m sorry Dorothy it isn’t me alone! But also mr David did it”(Samahani Dorothy sio mimi peke yangu na mr David Syndrome naye alishiriki)
“And how did you expect to be rich by doing that kind of a thing?”(Na mlitegemeaje kuwa matajiri kwa kufanya kitu cha namna hii?)
“By producing ZAT to lenghten sufferers lives”(Kwa kutengeneza dawa ya kurefusha maisha ya wagonjwa, ZAT)
“Oh my God so that is why you’re rich! Now I know why me and my brother came to the United Kingdom! We thought we came for studies but Unknowingly we came here to bring you the punishment! To bring you the pain you caused, God wanted you to feel how painful it is to suffer from AIDS. Now feel it! You and I gonna die the same kind of death!”( Mungu wangu! Kumbe ndio sababu nyie ni matajiri? Sasa ninaelewa ni kwanini mimi na kaka yangu tulikuja huku Uingereza! Tulifikiri tulikuja kusoma kumbe bila kujua tulikuja kuwaletea adhabu, kuwaletea maumivu! Mungu alitaka mjue ni kiasi gani kuugua Ukimwi inauma, mimi na wewe tutakufa kifo cha aina moja).
Suzanne alizidi kulia, maneno ya Dorothy yalimchoma sana moyoni mwake na hakuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kuendelea kumwomba msamaha!
“I’m sure even David Syndrome got it from Johnson so we all gonna die! Nobody is gonna escape this,may be profesor Owo!”(Nina hakika hata David Syndrome naye aliuopata kutoka kwa Johnson! Hakuna hata mmoja atakayepona, labda profesa Owo!)
*****
Hali ya Dorothy ilizidi kuwa mbaya ikalazimu naye akatishe masomo yake na kurejea Uganda ambako wala hakuchukua muda mrefu sana akawa amefariki dunia na kaburi lake lilichimbwa pembeni mwa kaburi la Johnson! Kabla ya kifo chake Dorothy akiwa taaban nyumbani kwao Kampala aliandika barua kuhusu siri juu ya ugonjwa uliosababisha vijana wengi wapoteze maisha yao nchini Uganda!
Barua ya Dorothy ilisambazwa Uganda nzima na hatimaye ilifika Tanzania ambako pia ugonjwa huo ulishaingia na kuua watu wengi, vijana wote waliowahi kuchanjwa chanjo hiyo waliingiwa na wasiwasi mkubwa na wengi waliendelea kuteketea kila siku zilivyozidi kupita!
Kifo cha Dorothy kilimsikitisha sana Suzanne na kilimpa simanzi kubwa sana na kumfanya ashindwe hata kufanya kazi zake vizuri! Ni kihoro na wasiwasi juu ya kifo ndivyo vilivyosababisha Suzanne augue mapema zaidi na miezi tisa tu tangu Dorothy afariki dunia Suzanne pia alifariki dunia kwa ugonjwa huo huo!
Dawa za kuongeza nguvu zilizotengenezwa katika viwanda vyake hazikusaidia kitu chochote kurefusha maisha yake.
Kifo cha Suzanne kutokana na Ukimwi kiliwasikitisha watu wengi sana nchini Uingereza na taarifa ziliposambaa duniani kuwa aliyetengeneza dawa ya kuongeza maisha alikuwa amekufa kwa ugonjwa ule ule watu wengi walishindwa kuiamini dawa yake hivyo manunuzi ya dawa ya ZAT yalishuka sana duniani kiasi kwamba kiwanda kiliingia katika hatari ya kufilisika.
Mawazo ya kufilisika yalimfanya David aanze kukonda na miezi michache tu baadaye alianza kupatwa na homa za mara kwa mara! Alitibiwa katika hospitali nyingi kubwa kubwa bila mafanikio, alianza kuhisi kitu kilichomsumbua na kuamua kuyatumia madawa yake ya kuongeza nguvu ili kurefusha maisha yake.
Yalimfanya aonekane ni mwenye afya kwa juu lakini ndani aliendelea kutafunwa taratibu na ugonjwa! David alijua maisha yake yalikuwa yamefikia mwisho na ndoto zake za kuwa tajiri kumzidi Bill Gate zilikuwa zimefikia kikomo.
Roho ilimuuma kupita kiasi na alijilaumu kwa uamuzi wake wa kutengeneza mdudu ambaye hatimaye alikuwa amerudi mwilini mwake kumuangamiza mwenyewe! David alilia na alipomfikiria profesa Owo huko Nigeria alishindwa kuelewa alikuwa na hali gani! Pia alivyomkumbuka swahiba wake Suzanne machozi yalimtoka.
Ndani ya nafsi yake alijisikia mkosaji mkubwa na alitamani asimame mahali Fulani juu angani na kuuomba msamaha ulimwengu mzima, kwa aliyokuwa ameyafanya, lakini aliogopa kwa kuhofia kushtakiwa kwa mauaji ya halaiki ya watu duniani nzima!
“Nitakufa kimya kimya!” Alijisemea David Syndrome moyoni mwake.
*****
Hali ya David ilizidi kuwa mbaya siku hadi siku na kuna kipindi alishindwa hata kwenda kazini kwake ni ugonjwa wa kuharisha uliozipunguza nguvu zake zaidi na kumfanya mara nyingi awe anashinda kitandani amelala, ukimwi ulikuwa ukimuua yeye mwenyewe aliyeutengeneza.
“Is Profesor Owo dying like me?”(Profesa Owo atakufa kama mimi?)Alijiuliza David.
*****
Siku Osama aliposhambulia minara ya jengo la World Trading Centre katika jiji la New York na jengo la Wizara ya Ulinzi la Marekani huko Washington, David Syndrome alikuwa ndani ya gari lake jirani kabisa na jengo la WTC! Hali yake ilikuwa mbaya mno na alikuwa amekata tamaa kabisa alichofanya ni kuandika barua ya kuiomba msamaha dunia na kukimbia kujitupa ndani ya moto wa jengo hilo.
Lakini aliokolewa baadaye na alipoongea na waandishi wa habari kuelezea ni kwanini aliamua kujiua ndipo alipoeleza waziwazi kuwa alikuwa ameua watu wengi sana duniani kwa virusi vya Ukimwi alivyotengeneza yeye na wenzake!
Dunia nzima ilipigwa na butwaa kusikia virusi vilivyokuwa vikiua watu Afrika ulitengenezwa na binadamu kwa lengo la kujipatia pesa.
Wiki chache baadaye David alihukumiwa kifo na kuchomwa sindano ya sumu na kufariki dunia! Serikali ya Uingereza ikaanza kazi ya kusaka mtu muhimu sana katika zoezi la kutengeneza virusi hivyo Profesa Owo! Wapelelezi walitumwa nchini Nigeria kufanya kazi hiyo.
****
Lagos Nigeria
Hakuna hata mtu mmoja aliyeijua siri ya utajiri wa Chifu Onuku, mtu aliyeaminika kuwa tajiri kuliko watu wote nchini Nigeria na utajiri wake ulitisha, hakuna mtu aliyejua kuwa tajiri huyo kabla ya kurejea Nigeria kutoka Uingereza aliitwa profesa Owo aliyekuwa akisakwa.
Alikuwa mfadhili mkuu wa serikali ya Nigeria alitoa na misaada mikubwa kwa watu wasiojiweza! Vituo vyake vya kupima magonjwa ya binadamu na pia hospitali zake zilitoa huduma bure Nigeria nzima kila siku ya alhamisi, siku ya Ijumaa aligawa mafuta ya taa bure katika vituo vyake vilivyotapakaa nchi nzima ya Nigeria!
Umaarufu wa mtu huyu nchini Nigeria ulikuwa mkubwa kumzidi hata rais wa nchi hiyo, hakuguswa na mtu yoyote hata alipofanya kosa lolote kisheria! Huyu ndiye profesa Owo aliyemtengeneza mdudu wa Ukimwi akiwa Uingereza akiwa na Suzanne pia David Syndrome!
Taarifa za kusakwa kwake zilimfikia kupitia matangazo ya redio na televisheni, alijua mwisho wake ulikuwa umefika hasa baada ya kusikia David Syndrome alihukumiwa kifo na kudungwa sindano ya sumu kwa kosa hilohilo.
“Hawanipati na wakinipata wao ni wanaume!” Alisema Profesa Owo au chifu Onuku kama alivyojulikana na wengi nchini Nigeria na siku iliyofuata alipanda ndege kuelekea Cambodia ambako alifanyiwa upasuaji na kuibadili kabisa sura yake, alichofanya ni kuutangazia umma kwamba alikufa katika ajali ya gari.
Maiti ya mtu mwingine tofauti ilinunuliwa na kuzikwa kama chifu Onuku, hakuna mtu aliyeruhusiwa kuiona maiti hiyo na mwezi mmoja baadaye profesa Owo alirejea kutoka Cambodia bila kutambuliwa na mtu na kutangazwa kama mrithi wa mali za marehemu wakati alikuwa ni yeye mwenyewe. Suala hilo alilifahamu mke wake peke yake.
*****
Wapelelezi kutoka shirika la kijasusi la Uingereza Scortland Yard waliotumwa nchini Nigeria kumtafuta profesa Owo, iliwawia kazi ngumu sana kumpata na walikaa Nigeria kwa miezi sita mizima bila mafanikio lakini hawakukata tamaa.

Je nini kitaendelea?
Tukutane kesho.
Unaweza kushare kwa ajili ya marafiki zako.

No comments