Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 01

 
“Kwani lazima ...kwani lazima mama Mei uvae hivyo? Kwa nini usivae gauni au sketi? Basi si bora hata ungevaa ile suruali yako kubwakubwa...mara hii umesahau kwa nini tupo hapa hapa ee!” alisema kwa kufoka baba Mei huku akimwangalia mke wake kwa macho yenye hasira... “Baba Mei kwani tatizo liko wapi? Mbona unakuwa na wivu wa kijinga... mimi ndiye ninayeweza kujichunga mwenyewe, nikitaka kuharibu nitaharibu mwenyewe,” alisema mama Mei huku akitoka, mkononi alishika mfuko wenye chupa tupu za bia... “Basi afadhali juu ungevaa blauzi kubwa kuliko hicho kidude,” baba Mei aliongeza kushauri... “Baba Mei bwana... kwani wewe hulisikii hili joto la Dar?” mama Mei aliongeza akiwa ameshafika hatua zaidi ya tano kutoka nyumbani hapo. Baba Mei alitoka na kusimama nje akimwangalia mke wake anavyotembea kwenda dukani na jinsi alivyogoma kusikia ushauri wake... “Hivi mama Mei ni lini atajitambua lakini? Ina maana mpaka sasa hajajijua kwamba ana umbo tata! Hajui kama hapa ni mjini?” alisema moyoni akiwa amejishika kiuno. *** “Nilikwambia ndugu yangu Sudi, mimi mkali wa drafti
lakini sijui ni kwa nini hutaki kuamini wewe,” alisema Jombi huku mlio wa kete ukitawala. Wengine waliokuwa wakushuhudia mchezo huo ni Mfaransa na Jumbe. Ilikuwa Jumamosi kwa hiyo hakuna aliyekwenda kazini na muda huo walishakula na kufika kwenye kijiwe hicho ambacho kina michezo mingine kama pool na bao. Mara kikapita kimya kama vile waliamrishwa kutulia... “Jamani yule mwanamke vipi?” alihoji Mfaransa... “Yule kahamia juzi pale kwa mzee Hewa...ana mume na mtoto mmoja...nasikia mume wake anafanya kazi Halmashauri ya Jiji,” alisema Jombi. Sudi yeye alibaki ametoa macho tu... “Tena mume wake dakika kumi nyuma alipita hapa na gari dogo jeupe,” aliongeza Mfaransa. Mama Mei alikuwa kama kituko, kwani mchana huo wa jua kali, yeye alivaa kanga kwa kuizungushia kiunoni, juu alivaa kitop ambacho kwa chini kilikuwa hakifiki usawa wa alipopitisha kanga. Hilo moja, pili, maumbile yake ya nyuma, yaani wowowo ni kama alikuwa anatumia dawa za Mchina ingawa ukweli ni kwamba, hakuwa mtumiaji wa dawa hizo zaidi ya Mungu kumjalia tu. Kama angepita mbele yako
akitokea upande mmoja kwenda mwingine, ungeweza kusema anataka kuinama ili aokote kitu kwa jinsi alivyokuwa amefungashia. Watu walikuwa wakisema umri wake wa miaka 31 na umbo lake ni vitu viwili tofauti. Kifuani alibanwa sana na kumfanya aonekane mwembamba. Mama Mei alijijua kuwa ana macho ya gololi hivyo alipomwangalia mtu yakiwa kama yanataka kusinzia kama siyo kulala, yalimzidishia urembo. Wakati anachumbiwa na baba Mei, karibia wanaume wengine wanne walikuwa wakimfukuzia, wawili walitaka kumuoa kabisa, wawili walitaka kupita tu ili kuchezea lakini msimamo wake ulibaki kwa baba Mei au Kitwana. Mara zote anapokwenda mahali akiwa amevaa suruali au sketi za kimini, watu huachana na shughuli zao kwa muda ili kumfaidi anavyopita mpaka kupotea. Hali hiyo imekuwa ikimfanya mumewe kupata gharama bila sababu kwani anaposema anakwenda mahali, au ampe pesa ya Bajaj au ya teksi kama hatampeleka yeye, lengo
likiwa kumkimbiza na macho ya watu. *** “Jamani! Jamani! Sasa kwa nini avae kanga vile wakati anajijua ana mzigo mkubwa?” alihoji Sudi sasa... “Ha! Yale ni maamuzi yao ndani ya familia bwana. Mtu umeambiwa ana mume na ametoka nyumbani halafu wewe unashauri asingevaa vile, sasa angevaaje kwa mfano?” alisema Mfaransa. “Angejistahi bwana...ona sasa... oneni wenyewe,” alisema Jumbe huku akimfuatilia mama Mei anavyotembea na kulitingisha wowowo lake. Vicheko vya kike kutoka kwenye baadhi ya nyumba za jirani vilisikika lakini ni hakika kwamba, waliokuwa wakicheka wote walikuwa wakimwangalia mama Mei kwa kupitia madirisha au milango. *** Siku iliyofuata ni Jumapili, Jombi aliamua kupita nje ya nyumba ya mzee Hewa ili kuona kama angeweza kumwona mama Mei... “Shikamoo mzee Hewa,” alisalimia Jombi...
“Marhaba Jombi, za siku nyingi bwana?” “Nzuri, upo mzee wangu?” alijibu Jombi huku akikaa kwenye kiti hapo nje... “Nipo bwana, karibu sana,” mzee Hewa alimkaribisha Jombi ambaye naye alikaa huku macho yakiwa mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Ni muda huohuo, mama Mei alitoka akiwa ameshika mfuko wa rambo wenye uchafu kwenda kutupa kwenye pipa pembeni ya nyumba. Siku hiyo pia alipiga kanga moja  tena nyepesi huku ndani akionekana kusindikizwa na skintaiti. Juu alivaa kiblauzi cha njano, kata mikono... “Habari yaka anko?” alimsalimia Jombi huku akipita karibu yake na kulitingisha wowowo kisawasawa kabisa... “Nzu...nzu...nzuri sista... mi...wewe vi...” alibabaika kujibu salamu Jombi. Mzee Hewa alimkazia macho mama Mei mpaka anavyotupa ule mfuko na kusema kwa sauti ya chini akimwambia Jombi...

No comments