Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 2

ILIPOISHIA “Nzu...nzu...nzuri sista...mi... wewe vi...” alibabaika kujibu salamu Jombi. Mzee Hewa alimkazia macho mama Mei mpaka anavyotupa ule mfuko na kusema kwa sauti ya chini akimwambia Jombi... SASA SHUKA NAYO MWENYEWE... “YAANI Jombi mwanangu sijawahi kupata majaribu kwenye nyumba hii kama mwaka huu...” “Kwa nini mzee Hewa?” Jombi aliuliza kwa sauti ya chini sana ili mama Mei asisikie kwani sasa alikuwa akirudi ndani. Na hata alipokuwa akirudi, vibastola vilitokeza kwa pembeni na kumfanya aonekane namna alivyojazia hata kwa mbele... “Loo! Kumbe si kwa nyuma tu, hata front,” Jombi alijisemea moyoni huku akimwangalia mwanamke huyo kwa jicho la wizi, akazama ndani... “We Jombi unavyoona unaweza kuishi na mwanamke wa hivi kwenye nyumba moja?” mzee Hewa aliuliza... “Kazi sana mzee Hewa...mimi hata kuishi nyumba jirani siwezi achilia kuishi naye nyumba
moja,” alisema Jombi akikiri uzuri wa mwanamke huyo. Baada ya dakika kama tano, baba Mei alitoka akionekana ana kasafari... “Wapi bwana?” mzee Hewa alimuuliza baada ya kumwona mkononi ameshika funguo za gari... “Nafika mjini mara moja... huyu nani mzee wangu?” aliuza baba Mei akitaka kumjua Jombi... “Huyu kijana wangu... anaishi mtaa wa pili kule... sasa amepita hapa akaona anisalimie kidogo mzee wake,” alijibu mzee Hewa... “Ahaa! Oke...halafu anaondoka zake?” baba Mei alitaka kujua zaidi... “Anaondoka...kwani vipi?” “Nimeuliza tu mzee wangu...” “Ataondoka...ataondoka.” Baba Mei alirudi kwanza ndani kisha baada ya kama dakika tano akatoka huku akisikika akisema... “Ole...ndiyo utanitambua mimi nani?!” Baada ya baba Mei kuondoka, mzee Hewa na Jombi walijadili lile swali... “Huyu bwana inaonekana amekutilia wasiwasi...maana kijana kama wewe kuja hapa
na mke mwenyewe kama huyu ni tatizo,” alisema mzee Hewa... “Hata mimi nimemshangaa hivyohivyo mzee Hewa kwani asingeweza kusema maneno yale mbele yangu huku nasikia...afadhali angekuuliza nikiwa sipo,” alisema Jombi huku moyoni yeye akiijua dhamira iliyompeleka pale... “Jana nilisoma gazeti moja linasema hizi nyumba zetu hapa zitabomolewa, we unazo habari hizi?” mzee Hewa alikata maongezi ya awali na kumuuliza Jombi hivyo... “Hapana mzee Hewa, ni kweli?” “Ngoja nikalilete na wewe upitie habari hizo,” alisema mzee Hewa huku akisimama kwenda ndani akiimba nyimbo za dini kama ilivyo kawaida yake. Mara, mama Mei alitoka. Safari hii alikuwa amejifunga kitenge, mkononi alishika kipochi kidogo, ilionekana alikuwa akienda dukani au gengeni. Licha ya kuvaa kitenge ambacho kilikaribia kuburuza chini lakini mzigo ulionekana kama kawa... “Anti naona unafuata bidhaa dukani sasa!” alisema Jombi. Mama Mei alimwangalia
kwa jicho la uchokozi kisha akasema... “Ni kweli lakini leo jua kali kama nini Mungu wangu, sijui niende na mwamvuli...” “Hata mimi nashauri hivyo maana...au nitume mimi.” Mama Mei alicheka huku akimkazia macho Jombi... “Yaani nikutume wewe anko si itakuwa dharau kubwa... nakwenda pale buchani na kwenye lile soko la pale kona...” “Nitume tu anti,” Jombi aling’ang’ania kutumwa. “Kweli?” mama Mei alitaka kujua ya moyoni... “Kweli kabisa anti,” alisema Jombi huku akisimama tayari kwa kutumwa... “Basi asante, nataka nyama kilo tano maana huwa naiweka kwenye friji kwa wiki nzima. Halafu nataka kabeji tatu... nazi sita...viazi mviringo kisado na mchele kilo tano,” alisema mama Mei... “Mh!” Jombi aliguna  moyoni baada ya kupata picha ya ukubwa wa mzigo atakaobeba. *** Jombi, licha ya kufanya kazi serikalini tena ya maana, pia ni mume wa mtu, bidhaa alizojituma kununua na maeneo zinakopatikana na nyumbani kwake ni jirani tu,
hivyo alikwenda kwa mahesabu sana. Alipokuwa kwenye soko alikumbana na maneno haya... “Baba Hawa leo umekuja mwenyewe? Mama vipi..?” “Leo baba Hawa nakuona umeamua kufuatilia mahesabu mwenyewe.” Mpaka mwisho anaondoka akiwa amebeba mfuko mkubwa kabisa, hivyo aliamua kuchukua Bajaj japokuwa alikokuwa anakwenda si mbali sana. *** Mzee Hewa alishangaa kukuta Jombi hayupo nje alikomwacha... “Kha! Huyu bwana vipi tena?” alijiuliza bila kupata majibu kwani hakumkuta mama Mei, aliingia ndani akijua anko huyo akirudi na mizigo atamwita. *** “Baba Hawa hiyo mizigo unaipeleka wapi mume wangu? Sikuelewi,” sauti ya mkewe, mama Hawa ilimshtua kwa nyuma akiwa anapanda Bajaj...
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma  Ijumaa ijayo.

No comments