Header Ads

Kigogo amjengea mjengo Vai wa Ukweli

Licha ya madai kuwa soko la fi lamu Bongo limeshuka na hivyo kutokuwa na faida kwa wasanii, muigizaji Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ anadaiwa kujengewa nyumba na kigogo anayetajwa kuwa ni mfanyabiashara, maeneo ya Mbezi-Msumi, jijini Dar.


 Chanzo cha uhakika kililiambia gazeti hili kwamba Vai wa Ukweli tangu awe na kigogo huyo maisha yake yamebadilika kwani muda mwingi anakuwa bize na kusimamia ujenzi wa nyumba yake hiyo ambayo hivi sasa imefi kia usawa na madirisha.

 “Vai yuko vizuri sana sasa hivi, maana muda mwingi anakuwa kwenye nyumba yake hiyo akiwasimamia mafundi kwa hiyo zile tabia za kupiga misele kwenye viwanja mbalimbali vya starehe siku hizi zimepungua.

 “Kuna habari kwamba anajengewa na kigogo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa madini hapa mjini maana si unajua fi lamu hazilipi na yeye mwenyewe hana kazi nyingine ya maana anayofanya,?” kilisema chanzo hicho.

 Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Vai wa Ukweli na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alijitetea kama ifuatavyo; “Jamani ni kweli ninajenga lakini sijengewi na mtu yeyote, watu waache umbeya, najenga kwa hela yangu mwenyewe ambayo nimeipata kwenye fi lamu na nyingine kwenye biashara zangu nyingine.”

 Hata hivyo, licha ya gazeti hili kutaka kufahamu kuhusu ‘biashara zake zingine’ ni zipi, muigizaji huyo alipotezea bila kutoa ufafanuzi.

CHANZO: GPL

No comments