Header Ads

Kigogo wa madini mkoani Mwanza alifika bei kwa Snura

Huku Wimbo wa Chura ukizidi kuwa gumzo baada ya serikali kuufungia, kuna taarifa kuwa, kigogo wa kampuni moja ya madini mkoani Mwanza, alifika bei kwa mtunzi wa wimbo huo, Snura Mushi, AMANI limeambiwa. Ishu hiyo ilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Malaika jijini Mwanza ambapo Snura na skwadi yake walikuwa wakitumbuiza.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kigogo
huyo aliyetajwa kwa jina moja la Maita, ‘alimfia’ Snura baada ya kumwona alivyoumbika hivyo kumtuma mpambe wake kusimamia zoezi la kumpata mwanadada huyo kwa kiasi chochote cha pesa. “Jamaa ana pesa, akamtuma mpambe ahakikishe Snura anapatikana, iwe kwa pesa au kwa kitu chochote atakachotaka. “Kuna wakati mpambe alikutana na Snura akishuka stejini, akamsalimia, Snura akaitika lakini kabla hajampa salamu za kigogo, walinzi wake walimchukua hadi nyuma ya steji,” kilisema chanzo  Ikazidi kudaiwa kuwa, zoezi la kumpata Snura liliendelea mpaka mwisho wa shoo lakini walinzi wake hawakutoa nafasi kwani walimwingiza kwenye gari na kwenda hotelini, kigogo huyo akaambulia namba ya simu aliyopewa na watu wa karibu na Snura. Ili kupata mzani wa habari hii, juzi, Amani lilimtafuta Snura na mazungumzo yalikuwa hivi: Amani: (baada ya salamu) kuna madai kuwa, ulipokuwa Mwanza, kigogo mmoja wa madini alifika bei, yaani alikutaka kwa kiasi chochote kile cha pesa, unazo habari? Snura: Mh! Mimi sijui lolote mbona. Amani: Hukuambiwa ukumbini? Snura: Unajua hata promota wangu alifurahi, mimi nipo tofauti na wengine. Nilikuwa napanda stejini nikimaliza kuimba nakwenda kukaa na walinzi wapo. “Shoo ilipoisha, niliingia kwenye gari nikaenda hotelini nilikofikia.

Kuna wenzangu walikwenda klabu mimi sikwenda.” Amani: Nasikia jamaa alipewa namba yako, hakuna mtu amekupigia? Snura: Wanaopiga simu kwa siku ni wengi kaka, mtu nikishajua mwelekeo wake nakata. Huenda alipiga.

Unajua mimi si kama wale wengine (hakuwataja majina).” Wiki iliyopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliifungia Video ya Wimbo wa Chura huku Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) likimtaka ajisajili kama mwanamuziki. Snura aliomba ladhi Wabongo na kujisajili Basata kisha kuirekebisha video hiyo.

CREDIT: AMANI

No comments