Header Ads

Lulu Diva: Mapenzi na Nay siyo ya mitandaoni


MWANADADA anayekuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa video queen Bongo, Lulu Abbasi ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa mapenzi yake na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ siyo ya mitandaoni hivyo hata akiweka picha ya mwanamke mwingine
hamuonei wivu.

 Ladiva aliyasema hayo baada ya hivi karibuni Nay wa Mitego kuweka picha ya mrembo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema ndiye ‘wife’, lakini mwanadada huyo alisema jambo hilo halimuumi na wala haoni wivu, labda angemkuta chumbani yangekuwa mengine.

 “Sikuona wivu kwa picha aliyoweka Nay kwa sababu mara nyingi hata mimi humuweka Wizkid maana namkubali sana ukiachana na mpenzi wangu, sikuwahi kumposti Nay mpenzi wangu, kwa sababu sipendi mapenzi ya kujianika mitandaoni,” alisema.
CREDIT: RISASI

No comments