Header Ads

Lulu Diva: Namuogopa Baraka Kama Ukoma


Lulu Abassi ‘Lulu Diva.

Muuza nyago (video queen) maarufu Bongo, Lulu Abassi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kudai kuwa akikutana na mkali wa Bongo Fleva, Baraka Andrew Odiero ‘Baraka Da Prince’ hawawezi kusalimiana kwani anamuogopa kama ukoma kwa madai kwamba alimchonganisha na mpenzi wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
barakaBaraka Andrew Odiero ‘Baraka Da Prince’
Akizungumza na Wikienda, Lulu Diva alisema kuwa Baraka alimpelekea Nay umbeya na kumtangazia ubaya kwa sababu waliwahi kuingia kwenye uhusiano lakini yeye aliamua kuachana naye kwa sababu aliona hawatafika mbali.
“Baada ya kuachana na Baraka, alianza kunitangazia ubaya kwa Nay kuwa sifai, kisa kikiwa ni kumpiga chini hivyo namuogopa kama ukoma,” alisema Lulu Diva.
Baraka alipotafutwa alimkana Lulu Diva kuwa hajawahi kuwa naye na wala hapendi kumzungumzia.

Chanzo: GPL

No comments