• Latest News

  May 07, 2016

  Lulu la Diva amanasa Wizkid

  MUUZA nyago anayepanda kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ hivi karibuni amefunguka kuwa hatimaye ametimiza ndoto yake ya muda mrefu aliyokuwa nayo ya kujiweka karibu na mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’.
   
   Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili, Lulu Diva alisema tangu ajikute ‘in love’ na Wizkid kila mara alikuwa akimtumia ujumbe au ‘kumtag’ picha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram hatimaye hivi karibuni mkali huyo wa Wimbo wa Ojuelegba alianza kujibu SMS zake jambo lililoanzisha safari ya kumnasa mkali huyo.

  “Najihisi kuwa na bahati sana duniani maana Wizkid ni kipenzi cha wanawake wengi, huwezi amini mara ya mwisho nachati naye aliniambia anakwenda kwenye tamasha Zambia na akirudi Nigeria aliniambia nikutane naye Lagos, so kwa sasa niko katika maandalizi ya kuelekea huko na bila shaka naye ameshavutiwa na mimi,” alisema Lulu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Lulu la Diva amanasa Wizkid Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top