Header Ads

Malaika amsamehe baba’ke

Sexy lady wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’, amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa amemsamehe baba yake mzazi ambaye huko nyuma hawakuwa katika maelewano mazuri tangu akiwa mdogo. 


Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Malaika, alisema kuwa kuna mambo ya kifamilia yalitokea huko nyuma hadi kufikia hatua ya kutokuwa na maelewano na baba yake lakini
kwa sasa ameamua kufungua moyo wake na kumsamehe mzazi wake huyo akiamini na vitu vingine vitafunguka kibaraka.

 “Nimemsamehe baba yangu ambaye nilikuwa na kinyongo naye kwa muda mrefu sana lakini sasa hivi moyo wangu ni mweupe kabisa na ninaamini kuwa na mambo yangu mengine yatafunguka kwa vile yeye ni mzazi niweze kupata baraka zaidi,” alisema Malaika.

No comments