Header Ads

MALKIA WA PEMBE' MCHINA ANAYEDAIWA KUENDESHA BIASHARA YA MENO YA TEMBO AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU DAR


KESI inayomkabili mwanamke mfanyabiashara ambaye ni raia wa China, Yang Feng Glan anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ujangili wa pembe za ndovu Barani Asia, imeahirishwa kusikilizwa leo Jumatatu katika Mahakama ya Kisutu Dar hadi baada ya wiki mbili zijazo.
Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa Pembe,anayeshutumiwa kuendesha biashara hiyo haramu kwa takribani miaka 14, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.
Yang Feng Glan amekana mashtaka hayo.
Mahakama imeambiwa kwamba faili ya kesi yake bado imo mikononi mwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma.
Maafisa wa Serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa.
Tanzania imepoteza theluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

No comments