Header Ads

Martin Kadinda: Petit Bado ni Mfanyakazi wa Endless Fame

Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema kuwa petit Man bado yupo Endless Fame Films.

Hivi karibuni kumeonekana kutokea ugomvi kati ya Petit na Mirror. Taarifa zimedai kuwa ugomvi huo umefanya mpaka agombane na bosi wa Endless Fame, Wema Sepetu japo siku chache alipofanya mahojiano na Bongo5, Petit alisema, “Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani.”

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Kadinda alisema kuwa ugomvi wa Petit na Mirror siyo mara ya kwanza kutokea.

“Petit bado yupo Endless Fame kwakuwa bado hajaiandikia barua kampuni kuwa anatoka na yote yaliyotokea kati ya Petit na Mirror au Wema ni tofauti zao tu kawaida ambazo si mara ya kwanza kutokea,” aliongeza.

Aidha Petit Man ameacha kumsimamia Mirror na sasa anafanya kazi na Nuh Mziwanda pamoja na Bill Nas.

No comments