• Latest News

  May 07, 2016

  Masogange, Rammy mahaba niue


  Muigizaji anayepanda kwa kasi Bongo, Rammy Galis ‘Pacha wa Kanumba’ na muuza nyago kwenye video za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ wamedaiwa kuwa katika mapenzi motomoto kiasi cha kushirikiana kila kitu!

   Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, kwa sasa kila unapomuona Masogange, Rammy naye anakuwepo, tofauti na zamani walipokuwa wakifanya kwa siri.
   “Kwa sasa siyo siri tena. Wanaonekana viwanja pamoja na hata juzikati wakati Rammy anatoka Sauz, Masogange alikwenda kumpokea na wakaoneshana mahaba niue pale airport,” kilisema chanzo chetu.

   Alipoulizwa Rammy kuhusu ishu hiyo, aliingia na kutoka: “Kwa nini unaniuliza hivyo? Hata kama ni kweli mimi sipendi haya mambo ya uhusiano yawe wazi, naogopa. Kwanza Agnes ni mshikaji tu.” Chanzo Kilimtafuta Masogange ili kumsikia anazungumziaje uhusiano huo ambapo alipopokea simu na kusikiliza madai hayo, aliguna, akakata simu na kuizima kabisa.
  CREDIT: RISASI JUMAMOSI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Masogange, Rammy mahaba niue Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top