Header Ads

MR FLAVOUR AMNYIMA USINGIZI RUBY

  Helen George ‘Ruby’
Mr Flavour

MWANADADA anayefanya vizuri kunako anga la Muziki wa Bongo Fleva, Helen George ‘Ruby’ amesema msanii wa Nigeria, Mr Flavour anamnyima usingizi, kwani ndoto zake ni kufanya naye kazi ili apae kimataifa.
Akibonga machache na paparazi wetu alisema, kila anapofikiria kupiga hatua kimuziki, linapokuja suala la wasanii wa nje, mtu anayetawala akili yake, akiamini kolabo yake itamfanya atusue ni Mr Flavour.
“Sikufichi, Mr Flavour ananinyima usingizi kwa jinsi ninavyomkubali, yaani jamaa anajua kupita maelezo, lazima nitafanya naye kolabo ‘soon’ ili nipate amani ya moyo, naamini kwa kiasi kikubwa nitapaa kimataifa kwa kazi tutakayoifanya na nafsi yangu itapoa,” alisema.

No comments