Header Ads

Mume wa Aaut Kumnyanga'anya mtoto Iyobo

Imevuja! Mume wa mwigizaji mahiri wa filamu za Kibongo, Aunt ezekiel, Sunday Demonte, huenda akaachiwa huru baada ya kusota gerezani, Abu Dhabi, Falme za Kiarabu alikofungwa tangu mwaka 2014. Demonte aliyefunga ndoa ya Kiislamu na Aunt Ezekiel, Novemba 2012, alitiwa nguvuni na polisi wa Dubai akikabiliwa na makosa kadhaa, likiwemo la kuishi nchini humo bila kuwa na kibali na kuhukumiwa kifungo jela. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa mwanaume huyo, Demonte anatarajiwa kuachiwa huru katika msamaha maalum unaotolewa kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kila mwaka, baada ya kuonesha tabia njema katika kipindi chote akiwa gerezani. 

“Amebadilika sana akiwa gerezani, muda wote yeye ni mtu wa kuswali, kutokana na tabia nzuri anayoionesha, serikali ya kule imeona bora na yeye aingizwe katika kundi la watu watakaoachiwa kwa msamaha maalum mwanzoni mwa Juni kabla ya mfungo kuanza,” kilisema chanzo hicho. Chanzo chetu kilizidi kutiririka kwamba, shauku kubwa ya Demonte atakapotoka jela ni kuonana na mkewe huku akisisitiza kwamba hajawahi kumpa talaka hivyo ni mkewe halali. 

“Anafurahia sana kutoka gerezani kama Mungu akimjalia lakini shauku kubwa ni kuonana na mkewe tena ili waendelee na maisha kwani anadai kuwa hajampa talaka na anampenda sana,” kilisema chanzo.Baada ya kupata ubuyu huo, Amani lilianza kumtafuta Aunt Ezekiel ambaye licha ya mumewe kuwa jela, kwa sasa anaminya kimalavidavi na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Mose Iyobo kiasi cha wawili hao kufikia hatua ya kupata mtoto. Jitihada za kumpata Aunt kupitia simu yake ya mkononi, hazikuzaa matunda, hali iliyomlazimu mwandishi wetu kumfungia safari mpaka nyumbani kwake. Sikia mazungumzo yao yalivyokuwa: Amani: Hivi una taarifa za kwamba Sunday anakaribia kutoka? Aunt: Ndiyo najua kwa sababu toka mwaka jana kulikuwa na taarifa hizo.


Amani: Kwa hiyo unazungumziaje kutoka kwake? Aunt: Daah sasa hapo mimi  nitazungumzaje? Tunamuomba Mungu amjalie atoke kweli. Amani: Kwa hiyo akitoka itakuwaje na wakati wewe sasa hivi mahabati yamekolea kwa Iyobo na mwenyewe anasema akitoka ataendelea na wewe haijalishi kama uko na mtu? Aunt: Yaani hiyo naomba tusubiri akitoka ndiyo tutajua, siwezi kuongea chochote kabla mtu hajatoka. Huko nyuma, Sunday aliwahi kuzungumza baada ya kupata taarifa kuwa Aunt amezaa mtoto na Iyobo na kusema kuwa hawezi kumuacha mkewe huyo kwa sababu mtoto amemzaa akiwa ni mkewe hivyo ataendelea kuwa naye na mtoto ni wake pia.

No comments