Header Ads

NAJMA AMSHANGAA GIGY

Msanii wa Bongo Fleva, Najma Datan ‘Naj’ anamshangaa Video Queen Gift Stanford ‘Gigy Money’ kwa kudai kuwa alimpigia simu, kisa wivu kwa mpenzi wake, Baraka Da Prince wakati hamjui yeye wala namba yake.

 Video Queen Gift Stanford ‘Gigy Money’.

 Akichonga  Najma alifunguka kuwa, hamjui Gigy anayesema kuwa alimpigia simu kumtahadharisha ukaribu wake na Baraka na
kwamba alimsingizia kwani hajawahi kuonana naye.
 
 Msanii wa Bongo Fleva, Najma Datan ‘Naj’ akiwa na mpenzi wake Baraka Da Prince.

 “Huyo Gigy atakuwa anatafuta kiki, sina mazoea na hao Ma-video queen na huyo Gigy simfahamu,” alisema Najma. Kwa upande wake Gigy alisema kuwa yeye amekuwa karibu na Baraka kama msanii mwenzake, alisikia Najma ana wasiwasi lakini hawezi kutafuta kiki kwa sababu anaweza kusimama mwenyewe.

No comments