Header Ads

Nauli za Mabasi yaendayo haraka ziko hapa, siku mbili bure


MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza rasmi viwango vya nauli ya mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam huku ikitoa leseni kwa kampuni itakayosimamia mabasi hayo.
Akitangaza nauli hizo mpya kwa umma jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2016, Mkurugenzi wa Sumatra, Gilliardi Ngewe amesema kuwa baada ya kupokea maombi na kisha kuyafanyia kazi wamekuja na kiwango hicho cha nauli kutokana na njia zilizopo kwenye barabara za mabasi hayo yaendayo haraka.

Ngewe alisema katika njia hizo kutakuwa na aina zaidi ya mbili ambazo zitakuwa na tofauti ya ulipaji wake ikiwemo ndefu ambayo ni (Trunk+Feeder route) yaani Morocco-Kimara hadi Mbezi, Tsh. 800 huku ile ndogo itakuwa ni (Feeder route ) ambayo ni Mbezi Kimara Tsh. 400.
Katika tukio hilo, Mkurugenzi wa SUMATRA, Gilliardi Ngewe alikabidhi Leseni maalum kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa ambapo alimtaka afanye kazi kwa mujibu wa sheria huku leseni hiyo ikiwa ni ya waka mmoja ambapo itaisha mpaka Mei 8, 2017,huku akieleza kuwa, UDA-RT wanayo haki ya kuongeza mkataba kadri watakavyoona inafaa baada ya muda wa leseni kuisha.

No comments