Header Ads

Nisha adaiwa kupangiwa nyumba mpya na kigogo

 MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kupangiwa nyumba na kigogo mmoja serikalini (jina kapuni) maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar.
 
Chanzo makini kimenyetisha kuwa, Nisha amehama maeneo ya Kijitonyama alipokuwa anaishi awali baada ya kigogo huyo kuhitaji usiri zaidi kwani Kijitonyama alishindwa kuwa anamtembelea mara kwa mara kufuatia nyumba aliyokuwa anaishi kuzungukwa na ‘waswahili.’


“Kigogo noma, hataki kujulikana ndiyo maana akaona amhamishie Mbezi Beach kwenye utulivu,” kilivujisha chanzo ambapo Nisha alipotafutwa alikanusha kupangishiwa na kudai alipanga mwenyewe. “Nimepanga mwenyewe jamani kwani mimi sina hela?” alisema.

Chanzo: GPL

No comments