Header Ads

Penzi la Kiba, Diamond lamtesa Jokate

Siri imevuja kuwa penzi la vinara wawili wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond PlanumZ’ na Ali Saleh Kiba ‘King’ linadaiwa kumtesa mlimbwende Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye amekuwa akijutia kujiingiza kwenye uhusiano na wasanii hao. 


 Mlimbwende Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

TUJIUNGE NA CHANZO
 Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Jokate, hivi karibuni alitupia mashairi ya Wimbo wa Ndi Ndi Ndi wa Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo baadhi ya mashabiki wake walimtaka kuwaahidi kuwa hatarudia kujiingiza kwenye penzi la mastaa hao (yaani Diamond na Kiba) kwani ishu hiyo ilimfanya atafsiriwe vinginevyo tofauti na ilivyokuwa awali. Ilisemekana kuwa kauli hizo za mashabiki hao zilikuwa kama kugongelea msumari wa moto kwenye kidonda kwani ishu hiyo imekuwa ikimsumbua na kumsababishia maumivu yanatokana na kujutia uamuzi wake huo kwa kuwa hakudumu nao. 
 
 Jokate akiwa na Ali Kiba.

“Unajua Jokate alijijengea na ana heshima sana kwenye jamii yetu kwa uwezo na upeo wake (IQ) na hata kujitambua, sasa anapokuwa na uhusiano na msanii kisha baada ya muda mfupi akaachana naye kama
ilivyokuwa kwa Diamond na sasa Kiba, inaweza kumshusha hadhi, na hiyo ndiyo inamfanya Jokate ajute kujiingiza kwenye mapenzi na mastaa hao,” kilifunguka chanzo hicho. 


ALIPASWA KUWA BUNGENI?
 Hata hivyo, baadhi ya watu wake wa karibu walikwenda mbele zaidi na kusema kwa muonekano wake alipaswa kuwa mjengoni (bungeni) akitema madini, kwani hawana hofu na elimu yake ila tatizo ni hilo tu la ‘kurukaruka’ na wasanii. “Kiukweli Jojo (Jokate) anastahili kuwa bungeni akitafuta njia mbadala ya kutatua matatizo ya wananchi wake wa jimbo lake f’lani hivi. “Au kama anataka kuendelea na mapenzi kwa kuwa ameachana na Kiba basi atafute mtu wake na kutulia naye kwani kuna baadhi ya warembo wenye majina wana watu wao na wametulia wanafanya mambo ya kujenga taifa,” alisema mmoja wa watu hao. 


HUYU HAPA JOKATE 
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Wikienda lilimtafuta mlimbwende huyo na kumfikishia madai hayo kisha kumweleza mabadiliko wanayotaka mashabiki na watu wake wa karibu ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Siku zote ninavyojua mimi mapenzi hayachagui, suala la kumpenda nani kwa maana ya staa, kiongozi, fukara, mwenye elimu au asiyekuwa nayo na wengineo ni matakwa ya moyo wangu kutokana na ulipodondokea. “Kama ni ishu ya kuwa bungeni ni suala la muda, wakati ukiwadia basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama ni mchumba wasubiri watamuona siku ya ndoa lakini hao wengine wala sijatoka nao!”
 
 KABLA YA DIAMOND, KIBA 
Ukiachilia mbali Diamond na Kiba, pia Jokate aliwahi kukiri na kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mbongo anayekipiga kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

No comments