Header Ads

Pete ya Uchumba ya Lulu gumzo!MSANII maarufu wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibua gumzo kubwa baada ya hivi karibuni kutinga kwenye Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar akiwa ametinga pete ya uchumba.
 Elizabeth Michael ‘Lulu’ akionyesha pete yake ya uchumba.

 Lulu akiwa ametinga kigauni chake kifupi cheupe alifikia kwenye ‘red carpet’ na kuanza kupigwa mapicha huku akiweka mapozi tofauti lakini kila pozi alilokaa alihakikisha pete hiyo inaonekana. “Hee, huyu Lulu kavishwa lini hii pete, na nani? Au ndiyo yule bosi wa redio?” alisikika akihoji mmoja wa wadada waliokuwa eneo hilo na kuwafanya wengine waanze kumjadili. Ndani ya ukumbi huo ilikuwa vigumu kuongea naye na alipopigiwa simu ili azungumzie undani wa pete hiyo hakupokea

No comments