Header Ads

Prezzo amfuata Gigy Bongo!

 IMEVUJA! Kumbe rapa mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’moja ya ishu zilizomleta Bongo ni pamoja na kukutana na muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford  ‘Gigy Money’. 

Akichonga na Over Ze Weekend Prezzo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Nipe Nikupe akimshirikisha staa wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ alisema kuwa, Gigy ni
msichana ambaye amekuwa akimsikia siku za hivi karibuni Wakenya wakimzungumzia hasa juu ya vituko vyake jambo lililomfanya kuvutiwa kuonana naye.


 “Gigy yuko hot mazee, nimemsikia sana Wakenya wakimzungumzia so nipo katika mpango wa kuonana naye, si unajua mimi nina mambo mengi, reality show na vitu vingine private,” alisema Prezzo. Gigy Money aliponyetishiwa ishu hiyo na Over Ze Weekend alifurahia jina lake kupaa hadi Kenya.

 Muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford  ‘Gigy Money’.
 

No comments