Header Ads

Rais wa Brazil Dilma Rousseff asimamishwa kaziRais wa Brazil aliyesimamishwa kazi na Bunge la nchi hiyo.
BUNGE la Seneti Brazil limepiga kura  kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo, Dilma Rousseff ambaye atasimamishwa kazi kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litachunguza tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili, kinyume cha sheria ya  fedha za serikali, kwa kuficha nakisi inayoongezeka ya umma kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma anazozikana.
Masenata 55 waliunga mkono   kura hiyo ya kutokuwa na imani naye dhidi ya kura 22 katika kikao cha zaidi ya saa 20.
Makamu wa Rais,  Michel Temer,  sasa atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.
Rousseff alichukua hatua ya mwisho kujiokoa kwa kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini humo kusitisha kura hiyo, lakini hatua hiyo ilipingwa.


CHANZO: BBC SWAHILI

No comments