Header Ads

Ruby naogopa kumuanika mwandani wangu


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayefanya poa, Hellen George ‘Ruby’ amesema kati ya vitu anavyoogopa duniani ni pamoja na kumuanika mwandani wake hadharani.

 Akipiga stori anayetikisa na ngoma zikiwemo Na Yule, alisema kuwa wanaume wengi wanakuwa katika uhusiano na msanii kwa sababu ya maslahi yao binafsi na pili kitendo cha kumuanika kinaweza kumfanya akazidi kuringa na kumpelekesha.

“Naogopa kweli kumuanika mwandani wangu, ujue unapomtangaza kuna watu wanakufitini ili wakupindue sasa kama hamjashibana ni rahisi kusikiliza maeneno ya watu, si hilo tu mwingine ukimuanika anajiaminisha basi anaanza kukupa masharti mara jukwaani usikatike sana,” alisema Ruby.

No comments